Home Habari za michezo BREAKING NEWS…UONGOZI SIMBA WAFANYA KUFRU..WACHEZAJI WAHAIDIWA MILIONI 750 ILI MSAUZI AFE USIKU...

BREAKING NEWS…UONGOZI SIMBA WAFANYA KUFRU..WACHEZAJI WAHAIDIWA MILIONI 750 ILI MSAUZI AFE USIKU HUU…


Simba usiku huu wana kazi moja tu ya kuhakikisha wanaiondoa Orlando Pirates kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika iwe kwa sare yoyote au ushindi.

Hiyo ni baada ya awali kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam walipowafunga wapinzani wao hao bao 1-0 ikiwa ni mechi ya kwanza ya hatua ya robo fainali ambapo kesho wanacheza mechi ya marudiano.

Haijalishi Orlando Pirates kujipanga wakiwa nyumbani lakini Simba chini ya kocha wao Pablo Franco wamejipanga kusonga nusu fainali ambayo licha ya kupiga hatua kubwa lakini watajizolea pesa nono kutoka CAF.

Matokeo yoyote mazuri yatakuwa na neema kwa nyota wa Simba kwani watavuna kiasi kikubwa cha fedha za bonasi waliozoahidiwa na uongozi wao.

Taarifa za uhakika ni kuwa miongoni mwa ahadi ambayo wameahidiwa ni kupewa zaidi ya asilimia 75 ya fedha za zawadi ambazo watazipata kutoka CAF kwa kutinga nusu fainali ambayo kila timu inayoingia inavuna kiasi cha Dola 450,000 (Sh1 bilioni).

Asilimia 75 ya Sh 1 bilioni ni takribani Sh750 milioni ambazo kama zikigawanywa kwa wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi la timu hiyo, kila mmoja ataweka mfukoni kiasi Sh18.7 milioni.

SOMA NA HII  UKUTA WA SIMBA WAWEKA REKODI MPYA BONGO..ONYANGO NA WAWA WATAJWA