Home Habari za michezo DAKIKA 90 ZA YANGA vs GEITA JANA HAZIKUWA RAHISI AISEE….ILIBAKI ‘KIDUNCHU’ TU...

DAKIKA 90 ZA YANGA vs GEITA JANA HAZIKUWA RAHISI AISEE….ILIBAKI ‘KIDUNCHU’ TU MENGINE YATOKEE…


Young Africans wametinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) baada ya kuitoa Geita Gold kwa  mabao 7-6 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa jana uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Geita walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 86 likifungwa na Offen Chikola na Shaban Djuma aliisawazishia Yanga dakika ya 90 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na ikapelekea kwenda kwenye Mkwaju wa Penalti.

Kwa Matokeo Yanga wametinga Nusu Fainali na watakutana mshindi kati ya Simba au Pamba kutoka jijini Mwanza mchezo utakaopigwa kati ya Arusha au Mwanza.

SOMA NA HII  KADUGUDA: - 'KAMA INAHITAJIKA MTU AFE ILI TUWE MABINGWA ..NIPO TAYARI...NITAFUNGUA TAWI AKHERA...'