Home Habari za michezo FIFA WALAINISHA KESI YA KANDA DHIDI YA MAZEMBE…WAIPA BARAKA MTIBWA…

FIFA WALAINISHA KESI YA KANDA DHIDI YA MAZEMBE…WAIPA BARAKA MTIBWA…


Mabosi wa Mtibwa Sugar, wamefafanua kitu gani kilicholifanya benchi la ufundi la timu hiyo kutomtumia winga nyota wa zamani wa TP Mazembe na Simba, Deo Kanda, lakini tayari mambo yamelainishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Mtibwa ilisema Kanda alishindwa kuitumika kwa vile kulikuwa na kesi FIFA baina yao na TP Mazembe, juu ya usajili wa Mkongo huyo wakisema ni mali yao na Mtibwa ikiamini ilimsajili kihalali na kudai haki zao katika shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa Mtibwa, Nassor Aboubakar alisema wiki mbili zilizopita FIFA iliwapa haki ya kumtumia Kanda kama mchezaji wao halali na kwa sasa wapo katika mchakato wa kushughulikia vibali vya kazi kabla ya kuanza kupiga kazi Ligi Kuu.

“Kanda anaweza akaanza mechi ijayo dhidi ya Dodoma Jiji inayopigwa wikiendi hii, Uwanja wa Jamhuri, naamini hadi kufikia muda huo tutakuwa tushakamilisha vibali vyake vya kazi,” alisema Aboubakar na kuongeza;

“Hiyo kesi ndio ilitufanya tusitishe kushughulikia vibali vyake vya kazi mapema, kwani tulisubiri maamuzi ya Fifa, ingawa Kanda alituhakikishia mapema alimalizana na TP Mazembe, sisi tulihitaji kujiridhisha.”

Alifafanua kuwa, Kanda aliendelea na mazoezi na timu ili kumjengea utimamu wa mwili, huku wakimjenga kisaikolojia kuzichukulia changamoto kama sehemu ya maisha.

SOMA NA HII  HALI YA KWA MKAPA IKO HIVI MUDA HUU SIO POA