Home Habari za michezo HASSAN DILUNGA ‘APIGWA KISU’ AFRIKA KUSINI….ISHU NZIMA IKO HIVI…PABLO ATOA KAULI…

HASSAN DILUNGA ‘APIGWA KISU’ AFRIKA KUSINI….ISHU NZIMA IKO HIVI…PABLO ATOA KAULI…


KIUNGO mshambuliaji fundi wa Simba, Hassan Dilunga, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki nne baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo.

Nyota huyo alipata majeraha ya goti wakati akiwa kambini na timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mhispania, Franco Pablo alisema kuwa kiungo huyo alifanyiwa oparesheni hiyo Afrika Kusini ambako alikwenda kwa ajili ya matibabu.

Pablo alisema kuwa anaamini kiungo huyo atarejea akiwa fiti baada ya kufanyiwa upasuaji huo huku akikiri kuwepo pengo lake katika shirikisho.

“Dilunga amefanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini na atakuwa nje kwa muda usiozidi wiki nne kabla ya kurudi tena uwanjani kuipambania timu yake.

“Dilunga aliumia goti la kulia Februari, mwaka huu katika mazoezi ya timu hiyo akijiandaa na mchezo dhidi ya Asec Mimosas.

“Kutokana na matibabu aliyofanyiwa huko, atakaa wiki tatu hadi nne, hivyo ninaamini atarejea akiwa fiti kwa ajili ya kuipambania timu yake,” alisema Pablo.

SOMA NA HII  RASMI...RAIS SAMIA AFUTA NYAYO ZA KAGAME..AAMUA KUMWAGA MAMILIONI MICHUANO YA CECAFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here