Home Habari za michezo KIPIGO CHA MADRID CHAMTIA KIWEWE TUCHEL….ADAI MCHEZO UMESHAISHA..AITOA CHELSEA…

KIPIGO CHA MADRID CHAMTIA KIWEWE TUCHEL….ADAI MCHEZO UMESHAISHA..AITOA CHELSEA…


TUMESHATOLEWA. Ndivyo alivyosema Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel, baada ya kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi Jumatano nyumbani Stamford Bridge.

Mabao matatu ‘hat trick’ ya Karim Benzema yameipa Real Madrid faida kuelekea mchezo wa marudiano Jumanne ijayo jijini Madrid.

Na Tuchel alipoulizwa kama gemu bado ipo, alijibu: “Hapana, mchezo umeshaisha.

“Tunatakiwa kukitafuta kiwango chetu kwa sababu tangu mapumziko ya kimataifa (tumepotea). Naogopa zaidi mechi ya Southampton wikiendi hii.”

Aliongeza: “Huwezi kutarajia matokeo kwa kiwango cha namna hii. Tunahitaji mabao matatu na mara ngapi hili limetokea? Tuwe wakweli.”

SOMA NA HII  ROBERTINHO AKOMAA NA KIKOSI CHA SIMBA AZIDISHA DOZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here