Home Habari za michezo KIPIGO KUTOKA EVERTON CHAMTIA WAZIMU RONALDO…AKWAPUA SIMU YA SHABIKI NA KUIVUNJA….

KIPIGO KUTOKA EVERTON CHAMTIA WAZIMU RONALDO…AKWAPUA SIMU YA SHABIKI NA KUIVUNJA….


Polisi wa Merseyside wamethibitisha kuwa wanafuatilia taarifa ya tukio ambalo Cristiano Ronaldo wa Manchester United anatuhumiwa kwa kuikwapua simu ya shabiki wa Everton na kuivunja.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea jana Aprili 9, 2022 baada ya Man United kufungwa bao 1-0 na Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park katika Premier League ambapo Ronaldo aliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ronaldo amesema anamkaribisha shabiki huyo kutembelea Uwanja wa Old Trafford wakati wowote United itakapokuwa inacheza. Shabiki huyo alikuwa akimpiga picha Mreno huyo wakati akirejea vyumbani baada ya mchezo.

SOMA NA HII  UWANJA WA MO SIMBA ARENA BUNJU SASA KIMEELEKEWA....KUTAJENGWA KAMA ULAYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here