Home Habari za michezo KISA KUITWA MZEE….RONALDO ASHINDWA KUMVUMILIA ROONEY…AMCHANA HADHARANI…

KISA KUITWA MZEE….RONALDO ASHINDWA KUMVUMILIA ROONEY…AMCHANA HADHARANI…


MSHAMBULIAJI wa Manchester United Cristiano Ronaldo amemjia juu Gwiji wa Manchester United na mchezaji mwenzake wa zamani Wayne Rooney akimuambia aache kumuonea wivu.

Hivi karibuni Wayne Rooney alinukuliwa akisema Manchester United haikustahili kumsajili Cristiano Ronaldo na Ronaldo pia hakusatahili kurudi Manchester United kutokana na kwamba Klabu hiyo sasa inatakiwa iwekeze kwa vijana kama kina Jadon Sancho na Marcus Rashford.

SOMA HAPA PIA:KISA MWENDO WA JONGOO WA RONALDO…ROONEY AVUNJA UKIMYA…AICHANA MAN UTD KWA KUMSAJILI…

Rooney aliendelea kusema kuwa Ronaldo wa sasa si wa zamani japo amejitahidi kufunga mabao muhimu kwa Manchester United mwanzoni mwa msimu lakini kwa maana ya uwekezaji wa miaka miwili au mitatu mbele Ronaldo hawezi kutegemewa.

Kwa upande wake Ronaldo amemjibu kwa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akisema “Una wivu sana.”

SOMA NA HII  MASAU BWIRE ALIA TIMU YAKE KUWA KWENYE NAFASI YA KUSHUKA DARAJA....ADAI LIGI IMEKUWA NGUMU KWAO...