Home Habari za michezo KISA MAYELE KUTETEMA JANA…KICHUYA AWEKA UNAFKI PEMBENI….AFUNGUKA KAZI ALIYOIFANYA…

KISA MAYELE KUTETEMA JANA…KICHUYA AWEKA UNAFKI PEMBENI….AFUNGUKA KAZI ALIYOIFANYA…


Kiungo Mshambuliaji kutoka Tanzania na Klabu ya Namungo FC Shiza Ramadhan Kichuya amesema hana budi kumpongeza Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Kichuya ametoa pongezi hizo, baada ya Mayele kutimiza ahadi yake ya kuifunga Namungio FC katika mchezo wa Ligi Kuu jana Jumamosi (April 23), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku bao lingine la klabu hiyo kongwe nchini likifungwa na Kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Kichuya amesema kama mchezaji na mwanamichezo hawezi kuwa mnafiki kwa kushindwa kumpongeza Mshambuliaji huyo kutoka DR Congo, kwani ni Mshambuliaji bora kwa sasa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

“Mimi sipendi kuwa mnafiki Mayele ni Mshambuliaji mzuri na anafunga kila mechi, kwenye mechi yetu alisema atafunga na si umeona amefunga, mtu akiwa anafanya vizuri lazima tutoe pongezi zake,” amesema Kichuya aliyeifungia Namungo FC bao la kufutia machozi dhidi ya Young Africans.

Baada ya kufunga katika mchezo wa jana Jumamosi (April 23), Mayele amefikisha mabao 12 akiwaacha washambuliaji wazawa George Mpole (Geita Gold FC) na Reliant Lusajo (Namungo FC) wakiwa na mabao 10 kila mmoja.

Hadi sasa Mayele hajazifunga Simba SC na Mbeya City katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Msimu huu, huku Young Africans ikitarajiwa kucheza dhidi ya Mtani wake Jumamosi (April 30), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Je Mayele atafanikiwa kuifunga Simba SC siku hiyo?

SOMA NA HII  KUMEKUCHA FEI TOTO ATAKA KULIANZISHA TENA AZAM, ADAI HANA FURAHA