Home Habari za michezo KUELEKEA ‘KARIAKOO DABI’….MAYELE AJIAPIZA KULIPIZA ALIVYOZALILISHWA NA HENOCK…’NITALIPAA’…..

KUELEKEA ‘KARIAKOO DABI’….MAYELE AJIAPIZA KULIPIZA ALIVYOZALILISHWA NA HENOCK…’NITALIPAA’…..


Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo na Klabu ya Yanga aliyejizolea umaarufu kwa staili yake ya ushangiliaji, Fiston Mayele ‘mzee wa kutetema’ amesema ana Deni la kuzifunga katika Ligi Kuu msimu huu Klabu ya Simba na Namungo.

Mayele amezungumzia pia kitendo Cha Beki wa Kimataifa wa DR Congo,Henock Inonga kumsindikiza nje wakati akifanyiwa Sub kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopita Kati ya Simba SC na Yanga na kusema kuwa hajui beki huyo alikuwa anafikiria Nini kufanya vile ila Kwake Ni deni na atalilipa.

Simba SC na Yanga SC zinatarajiwa kukutana kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara April 30 Mwaka huu.

SOMA NA HII  MBADALA WA MIQUISSONE AREJEA SIMBA...HITIMANA NI FULL SHANGWE...