Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WASAUZI KESHO KUTWA…SIMBA WAWEKA TUMAINI LAO KWA LWANGA…

KUELEKEA MECHI NA WASAUZI KESHO KUTWA…SIMBA WAWEKA TUMAINI LAO KWA LWANGA…


Simba wana jambo lao msimu huu kwenye mechi za kimataifa, ikiwa kwa sasa inahitaji sare tu katika mechi ya marudiano dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini ili itinge nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika kuhakikisha wanaenda kukamilisha jambo lao Sauzi, kocha mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco ameamua kumfungia kazi kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga ili arejee katika makali yake kwa kazi maalumu kwenda kuiua Orlando.

Lwanga alikuwa yupo nje kwa muda mrefu baada ya kuumia goti, lakini alirejea kwenye mechi tatu zilizopita ikiwamo ya kwanza dhidi ya Orlando ambapo Simba ilishinda bao 1-0, lakini kiungo huyo kutoa Uganda hakuwa kwenye ubora wake.

Juzi Jumanne katika mazoezi ya timu hiyo, kocha Pablo aliamua kumpigisha tizi Lwanga, licha ya wachezaji wengine waliocheza mechi ya kwanza kupumzishwa, ikiwa ni kama mbinu za kumuweka tayari kwa vita ya Johannesburg.

Katika mazoezi hayo, Pablo alitengeneza nusu uwanja ambao upande mmoja aliwaweka Taddeo Lwanga, Clatous Chama, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Yusuph Mhilu na Mzamiru Yassin na mwingine aliwaweka Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Israel Mwenda, Kennedy Juma na Joash Onyango.

Kwenye zoezi hilo wachezaji walikuwa muda wote wanaucheza mpira bila kutegea kwa vile wote walikuwa wanashambuliana na ndipo Matola alikuwa na kazi ya kumuangalia Lwanga.

Kiungo huyo Mganda ni kama aligundua kazi anayopewa ni maalumu, naye wala hakuwaangusha benchi hilo la ufundi, kwani alikuwa anafanya kila anachoelekezwa huku wepesi ukiongezeka katika kukaba na kuisogeza timu mbele.

SOMA NA HII  ALLY KAMWE ATAMBA, UONGOZI NAO WAWATAJA WAPINZANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here