Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO…SHEIKH MNGAZIJA AFICHUA HAYA KUHUSU AFYA ZA WACHEZAJI YANGA…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…SHEIKH MNGAZIJA AFICHUA HAYA KUHUSU AFYA ZA WACHEZAJI YANGA…


Daktari Mkuu wa kikosi cha Young Africans Sheikh Mngazija amesema wachezaji wote wa klabu hiyo wapo sawa kiafya na wanaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.

Miamba hiyo ya Soka la Bongo itapambana katika mchezo wa mzunguuko wa 21 wa Ligi Kuu msimu huu kesho Jumamosi (April 30) Uwanja wa Benjamin Mkapa, saa kumi na moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Daktari Mngazija amesema hali ya wachezaji wote wa Young Africans ipo shwari na kilichobaki ni kwa Kocha Nabi kufanya maamuzi ya kumtumia mchezo gani kwenye mchezo dhidi ya Simba SC.

“Wachezaji wote wapo salama, wana hali nzuri kiafya na wanaendelea na mazoezi ya kuikabili Simba SC Jumamosi, Kocha atakua na chaguo lake mwenyewe la kumtumia nani na nani asimtumie kwenye mchezo wetu ujao.”

“Kwa hiyo niwatowe hofu Mashabiki wa Young Africans kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba SC, hakuna mchezaji yoyote mwenye matatizo ya kiafya jamani, tupo sawa sawa na kila mchezaji anaweza kucheza mchezo wa Jumamosi.”

Young Africans kesho itaingia Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 54 ambazo zinawapa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Simba SC inayotetea ubingwa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo huo, ikiwa na alama 41, ambazo zinaifanya kuwa nyuma kwa alama 13 dhidi ya Young Africans.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUNGIWA VIOO KUCHEZA YANGA...KOCHA KASEMA NI MUKOKO NA MAYELE TU..AFUNGUKA KILA KITU...