Home Habari za michezo KUELEKEEA MECHI YA CAF…PABLO MJANJA SANA AISEE…KAWAPIGA CHENGA YA MWILI WASAUZI MCHANA...

KUELEKEEA MECHI YA CAF…PABLO MJANJA SANA AISEE…KAWAPIGA CHENGA YA MWILI WASAUZI MCHANA KWEUPE..


KOCHA wa Simba, Pablo Franco mjanja sana kwani juzi aliamua kuwazuga wapinzani wao wa michuano ya CAF, Oralndo Pirates ya Afrika Kusini baada ya kuanzisha kikosi cha wachezaji wengi wa akiba wakati wakivaana na Polisi Tanzania na kutoka suluhu.

Katika pambano hilo la Ligi Kuu Bara lililopigwa kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa, Pablo aliwapumzisha nyota wengi wa kikosi cha kwanza na kuanzisha wachezaji ambao hawatumii sana katika mechi za mashindano.

Pablo alimwanzisha kipa Beno Kakolanya langoni, huku beki wa kushoto alimpanga Gadiel Michael na Kennedy Juma na Pascal Wawa walisimama katika beki ya kati, huku Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin walicheza eneo la kiungo kuchukua nafasi za Jonas Mkude na Sadio Kanoute na Yusuph Mhilu alicheza katika nafasi ya Pape Ousmane Sakho.

Ilionekana kama Pablo alikuwa akiwazuga Orlando iwapo waliifuatilia mechi hiyo kuwasoma, kwani hata kipindi cha pili alifanya mabadiliko madogo kwa kuwaingiza kina Bernard Morrison, Sakho, Mkude na Jimmyson Mwanuke ambao walipambana kukabiliana na wenyeji waliocheza soka tamu na kuwabana Simba kwa muda mrefu.

Simba inajiandaa kuvaana na Orlando Jumapili ya wikiendi hii kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Matokeo ya jana yameifanya Simba kufikisha pointi 41 kutokana na mechi 19 na kupunguza pengo la pointi baina yao na Yanga kuwa 10, kwani watani wao wana pointi 51 kupitia mechi 19 pia.

Polisi itajilaumu kushiondwa kutoka na ushindi katika mchezo huo, kwani ilipoteza nafasi nyingi za wazi kupitia washambuliaji wao, Daruwesh Saliboko, VItalis Mayanga, Tariq Seif na Kassim Shaaban.

Mabadiliko ya kipindi cha pili yalizifanya timu zote kuongeza kasi na Simba ilionekana kuchangamka zaidi kutokana na Morrison na Sakho kuisumbua ngome ya Polisi na kumpa kazi, kipa Metacha Mnata.

Wenyeji hao kwa sare hiyo imechupa kwa nafasi moja kutoka ya tisa hadi ya nane kwa kufikisha pointi 24 baada ya mechi 19.

SOMA NA HII  MBADALA WA ONYANGO SIMBA HUYU HAPA....JAMAA ANAKABA MPAKA PUMZI AISEE...

Kocha Pablo alisema timu yake iliangushwa na ubovu wa uwanja, lakini alishukuru kupata pointi moja ugenini, huku kocha msaidizi wa Polisi George Mketto alisema bahati imewaangusha.

“VIjana wamecheza vizuri, japo tumeshindwa kutumia nafasi tulizopata, tunajipanga kwa mechi zetu zijazo,” alisema Mketto.

Vikosi vilivyoanza:

SIMBA: Kakolanya, Kapombe, Gadiel, Kennedy, Wawa, Nyoni, Bwalya, Mzamiru, Kagere, Mugalu na Mhilu

POLISI: Metacha, Datius, Mbegu, Bakar, Mmanga, Simba, Saliboko, Cosmas, Tariq, Mayanga na Shaaban.