Home Habari za michezo KWA TAARIFA YAKO…MAYELE NA KAGERE NI KITU KIMOJA…WOTE WAZEE WA KUTETEMA ,...

KWA TAARIFA YAKO…MAYELE NA KAGERE NI KITU KIMOJA…WOTE WAZEE WA KUTETEMA , WABAYA WA DK ZA JIONI…


Unaikumbuka ile mechi aliyokaa Ramadhan Kabwili langoni kwa mara ya kwanza akiwa langoni? Ilikuwa ni Februari 16, 2019 ni Kagere aliweza kumtungua na kutetema mbele ya watani hao wa jadi.

Kibao kikaja kugeuka pia walipokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa, Septemba 25,2021 ni Mayele aliweza kumtungua Aishi Manula kisha akatetema kwa mtindo wake ambao ni pendwa kwa sasa kwa mashabiki.

Wao na penalti

Jukumu la kupiga penalti huwa linakuwa miguuni mwa Kagere kwa kuwa kwenye mabao 7 ambayo amefunga, alifunga moja kwa penalti mbele ya Tanzania Prisons.

Pia alikosa penalti moja mbele ya Biashara United ilikuwa Uwanja wa Mkapa huku kwa upande wa Mayele yeye kwenye mabao 11 aliyofunga hakuna hata bao moja la penalti.

Lakini Mayele alisababisha penalti moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mkapa na mtupiaji alikuwa ni Shaban Djuma.

Watupiaji mabao muhimu jioni

Nyota hawa wawili ni wakali kwenye mabao ya usiku ambayo huwa yanakuwa muhimu kwa ajili ya timu hiyo kusepa na pointi tatu.

Kagere alicheka na nyavu mara mbili, alitupia mbele ya Namungo dk 90+4, Simba ilishinda bao 1-0 na mbele ya Coastal Union dk 90+3 ubao ulisoma Coastal Union 1-2 Simba.

Ilikuwa mechi dume mbele ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex ubao ulipokuwa ukisoma Azam FC 1-1 Yanga mpaka dk ya 76 ilipogota ile ya 77 Mayele akazamisha mpira nyavuni kisha akaomba atoke kwa kuwa alikuwa amepata maumivu.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here