Home Habari za michezo RASMI….HATIMAYE KELVIN JOHN AWEKA REKODI NYINGINE ULAYA…ACHUKUA NAFASI YA MJAPANI…

RASMI….HATIMAYE KELVIN JOHN AWEKA REKODI NYINGINE ULAYA…ACHUKUA NAFASI YA MJAPANI…


Kinda wa Kitanzania Kelvin John (19) baada ya kupandishwa kucheza timu ya wakubwa ya KRC Genk ya Ubelgiji, hatimae jana alipata nafasi ya kuichezea kwa mara ya kwanza katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Eupen katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Kelvin John katika mchezo huo aliingia akitokea benchi dakika ya 81 kuchukua nafasi nafasi ya Mjapan Junya Ito na kwenda kumalizia dakika 9 zilizokuwa zimesalia ili kukamilisha dakika 90 za mchezo.

“Nashukuru sana mashabiki kwa sapoti nikicheza mchezo wangu wa kwanza KRC Genk, nafuraha sana asanteni wote” amesema Kelvin John baada ya mchezo kumalizika

SOMA NA HII  MO DEWJI AIAMBIA DUNIA KUHUSU SIMBA..ADAI ANAPOTEZA PESA NYINGI NA KUPATA HASARA