Home Habari za michezo A-Z JINSI YANGA NA SIMBA ZILIVYOPAPATUANA BILA KUTOBOANA JANA…YANGA YAENDELEZA UBABE….

A-Z JINSI YANGA NA SIMBA ZILIVYOPAPATUANA BILA KUTOBOANA JANA…YANGA YAENDELEZA UBABE….


PAMBANO la watani wa jadi kati ya Yanga ambaye alikuwa mwenyeji na Simba limemalizika kwa matokeo ya sare ya bila kufungana ikiwa ni pambano la raundi ya pili ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na ufundi mwingi lakini pia uchache wa nafasi za mabao umelalamikiwa na wadau wengi wa soka kuwa ulikuwa ni mchezo ambao timu zote ziliangalia matokeo baada ya mchezo kuliko matokeo ndani ya mchezo, kwa maana zilicheza kwa tahadhari ya kuogopa matokeo ambayo yangeweza kupatikana mwisho wa mchezo

Kutokana na matokeo hayo klabu ya Yanga inaendelea kujikita kileleni ikiwa na jumla ya alama 55 ikifuatiwa na mahasimu wao klabu ya Simba ambayo ina jumla ya alama 42 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Baada ya mchezo huu klabu ya Yanga inatarajiwa kwenda mkoani Kigoma kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Ruvushooting unaotarajiwa uchezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

SOMA NA HII  MZEE DALALI ATAKA WANAOWANIA UBOSI SIMBA WAFUNGUKE WATAKAVYOIFUNGA YANGA TU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here