Home Habari za michezo BAADA YA KUISHINDWA SIMBA JUZI….YANGA WAPAA KWA HASIRA ZOTE KWENDA KIGOMA…

BAADA YA KUISHINDWA SIMBA JUZI….YANGA WAPAA KWA HASIRA ZOTE KWENDA KIGOMA…


Klabu ya soka ya Yanga imeanza safari kuelekea mkoani Kigoma kuikabili Ruvushooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC unaotarajiwa kuchezwa Mei 4 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

Yanga inakutana na Ruvu shooting ikiwa kinara kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na jumla ya alama 55 alama 13 zaidi ya Simba iliyopo katika nafasi ya pili ikiwa na mchezo mkononi.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulimalizika kwa klabu ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 3-1 mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Klabu ya soka ya Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kutoka kudondosha alaama kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya mahasimu wao Simba uliomalizika kwa sare ya bila kufungana huku ukiwapunguzia kasi ya kuelekea kuchukua ubingwa wao wa mara ya 28 wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA WA YANGA AWEKA WAZI MIPANGO YAKE, ATAJA SIFA ZA WACHEZAJI ANAOWATAKA