Home Habari za michezo BAADA YA KUONA JITIHADA ZAKE HAZIFUI DAFU….PABLO AIKATIA TAMAA SIMBA…ADAI HAWEZI KUBADILISHA...

BAADA YA KUONA JITIHADA ZAKE HAZIFUI DAFU….PABLO AIKATIA TAMAA SIMBA…ADAI HAWEZI KUBADILISHA HALI ILIYOPO…


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameonekana kuisikitikia timu yake ya Simba na kusema wachezaji wake wanaonekana kushindwa kabisa kupambana inapocheza na timu za katikati au juu ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akisema ni jambo lisilopendeza kwa klabu kubwa kama hiyo.

Wakati akiongea hayo, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro, amelalamikia umakini kwa wachezaji wa Kitanzania, akidai kama wangekuwa makini kidogo, basi mechi ya juzi dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba timu yake ingeondoka na ushindi na wala isingekuwa sare ya bao 1-1.

Makocha wote wawili waliongea hayo baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya raundi ya 25 ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku Pablo akionekana kukikatia tamaa kabisa kikosi chake akisema anafikiri sasa kimedhohofika kabisa kimwili na kiakili.

“Uhalisia ni kwamba hatuchezi vizuri tunapokuwa ugenini, sina ninachoweza kubadilisha kwa jambo hilo. Kiwango cha wachezaji wangu kilikuwa chini sana, siyo kiungo tu pekee, ila timu nzima, mistari yote, kuzuia, kushambulia, na hata mipira ya kutenga, nafikiri kwa sasa tumedhohofika kabisa kimwili, na kiakili, leo (juzi) hatukuwa sawa kabisa na hatukuwa na tamaa ya ushindi ukilinganisha na mechi zilizopita,” alisema kocha huyo raia wa Hispania na kuongeza.

“Baada ya dakika 60 tulisambaratika kabisa, tuko kwenye wakati mgumu, mara kwa mara tunakabiliwa na majeruhi na hicho ndicho kiwango chetu cha sasa, kila tunapokabiliana na timu za katikati na juu ya msimamo tumeshindwa kabisa kupambana, bila shaka haitoshi kwa klabu kubwa kama Simba,” alilalama Pablo.

Naye Minziro aliwalalamikia wachezaji wake kutokuwa makini kwani waliikamata mechi na hawakustahili kutoka sare.

“Nikiri tumepambana na timu kubwa na zuri, ila umakini kwa wachezaji wetu wa Kitanzania bado, wachezaji wangu wangekuwa makini wangeweza kufunga mabao mawili au matatu mwishoni mwa mchezo. Walishindwa kumalizia mipira, tungekuwa makini hii mechi ya leo (juzi) isingekuwa sare, tungeshinda,” alisema Minziro.

SOMA NA HII  KIGOGO SIMBA AMTABIRIA MAKUBWA INONGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here