Home Habari za michezo BAADA YA NTIBAZONKIZA ‘KUSEPESHWA’ YANGA…MAYELE AFICHUA MENGINE YA SIRI BAINA YAO WAWILI…

BAADA YA NTIBAZONKIZA ‘KUSEPESHWA’ YANGA…MAYELE AFICHUA MENGINE YA SIRI BAINA YAO WAWILI…


Baada ya Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Saidi Ntibazonkiza kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili ndani ya klabu ya Yanga jana Mei 30, 2022.

Nyota waliokipiga na mchezaji huyo ndani ya Yanga wameonesha masikitiko yao kumkosa mchezaji huyo ambae hajaongeza mkataba na Klabu hiyo.

Miongozi mwa nyota wa Yanga alioonesha kuguswa na kuondoka kwa Saido ni mpachika mabao kinara ndani ya Klabu hiyo, Mkongo Fiston Mayele ambae wamecheza pamoja msimu huu.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagrama Mayele ameandika;

“@ntibazonkizasaidi Nakutakia kila la kheri najua sio mwisho wetu kwa sababu ulikuwa unamchango mkubwa kwangu ntaendelea kukukumbuka ntakumiss sana najuwa tutaendelea kuwasiliana lakini bado ulikuwa unaumuimu kwangu nakupenda kaka yangu”

Mayele na Ntibazonkiza ndio vinara wa upachikaji mabao ndani ya kikosi cha Yanga ambapo mpaka inakamilika raundi ya 25, Mayele amepachika magoli 14 ya Ligi na Saido magoli 7.

SOMA NA HII  MADEAMA MAPEMA SANA HUKU WAKIMKOSA MWAMBA HUYU DHIDI YA YANGA