Home Habari za michezo DEWJI AVUNJA UKIMYA SIMBA…ADAI TIMU INAMAPUNGUFU KIBAO…..AKATAA SAJILI ZENYE SIASA…

DEWJI AVUNJA UKIMYA SIMBA…ADAI TIMU INAMAPUNGUFU KIBAO…..AKATAA SAJILI ZENYE SIASA…


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba SC Kassim Dewji amekiri mapungufu yaliyoonekena kwenye kikosi cha klabu hiyo kwa msimu huu 2021-22 ambao unaelekea ukingoni, huku klabu hiyo ikiuweka rehani Ubingwa wa Tanzania Bara.

Simba SC inatetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo, huku ikiachwa kwa alama 12 na Young Africans inayoongoza msimamo wa Ligi hiyo kwa kumiliki alama 55.

Kassim Dewji amesema kamati yake imeona mapungufu ya kikosi cha Simba SC msimu huu, hivyo kuna kazi kubwa ya kufanya ili kukipa nguvu kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi na kurejesha makali kama ilivyokua misimu minne iliyopita.

“Simba ya msimu huu tumeiona nafikiri sio siri tena kwamba kipi kinatakiwa kufanyika ili tupate timu bora kwa msimu ujao, hatukuwa na washambuliaji bora kama misimu michache iliyopita, kuna vijana wetu wamepungua ubora, lazima klabu ipate nguvu mpya.”

“Msimu huu asilimia kubwa ya mabao yetu tumekuwa tukiyapata kwa viungo na sio washambuliaji, washambuliaji wetu walifunga lakini mabao machache sana, isingekuwa rahisi kutinga hatua ya nusu fainali au hata fainali ya CAF.”

“Huu sio wakati tena wa kusikia mambo ya siasa Simba SC imeshatoka huko, tuanze sasa kuishi kwa hesabu zinazokamilika na watu wakaona hapa kuna hatua kubwa inapigwa, tunatakiwa kurudi kwa nguvu msimu ujao.” Amesema Kassim Dewji

Simba SC jana Jumanne (Mei 03) ilicheza mchezo wa Mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC mjini Lindi na kuambulia matokeo ya sare ya 2-2, huku mabao ya Mnyama yakifungwa na Beki wa Pembeni Shomari Kapombe na Kiungo Mshambuliaji Kibu Denis.

SOMA NA HII  UNAKUMBUKA USHINDI WA 4-3 WALIOPATA AZAM FC JANA...BASI HAYA NDIYO YALIYOTOKEA ...