Home Habari za michezo ISHU YA PABLO KUTAKIWA ORLANDO PIRATES…SIMBA WATOA TAMKO…TYR AGAIN AMPA ‘UHURU WA...

ISHU YA PABLO KUTAKIWA ORLANDO PIRATES…SIMBA WATOA TAMKO…TYR AGAIN AMPA ‘UHURU WA KUSEPA’….


WIKI chache baada ya kuing’oa Simba kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imemtangazia ofa nono kocha Pablo Franco kwenda kuchukua nafasi ya Mjerumani Josef Zinnbauer wanayetaka kumtimua klabuni.

Taarifa kutoka Sauzi zinasema uongozi wa Orlando ulianza kuonyesha nia ya kumtaka Pablo kabla ya kukutana katika michezo miwili ya Kombe la Shirikisho Afrika na timu hiyo kushinda kwa penalti 4-3 baada ya matokeo ya jumla kuwa bao 1-1.

Inaelezwa kwa nyakati tofauti mabosi wa Orlando walifanya mazungumzo na Pablo na kuweka ofa yao ikiwemo kumuonyesha nyumba ya kifahari atakayofikia iwapo atakubali kujiunga nao, kuboreshewa mshahara kutoka Dola 14,000 (karibu na Sh32 milioni) anaolipwa Simba hadi 25,000 (karibu Sh58 milioni) kwa mwezi.

Hawakuishia hapo walimueleza watampatia mkwanja wa usajili endapo watakaa na kukubaliana huku wakimboreshea kikosi kwa masuala ya kiufundi atakayokuwa anahitaji ikiwemo kuleta msaidizi wake mwingine.

Inaelezwa hadi sasa Pablo bado hajafanya uamuzi kama atimke Msimbazi au la, japo inadaiwa ameshaujulisha uongozi juu ya kutaka kuboreshewa masilahi kadhalika huenda lolote linaweza kutokea kulingana na ofa ilivyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alipoulizwa jana alisema uongozi haujapokea barua wala taarifa rasmi kutoka Orlando juu ya kumhitaji kocha huyo.

Try Again alisema taarifa za Orlando kumtaja Pablo wanaziona mitandaoni na hakuna jambo lolote rasmi kama ilivyo taratibu za usajili, huku akisema bado ana mkataba na Simba ila yeye ndiye mwamuzi wa mwisho kama atakubali kumalizana na Orlando.

“Suala la kocha kuondoka anapopata timu nyingine ni tofauti kwani anaweza kulimaliza mwenyewe kabla ya kuja kwetu kukamilisha taratibu ila mchezaji mwenye mkataba lazima uongozi wa timu husika wafahamu anahitajika na timu nyingine ndio wapewe ruhusa ya kuzungumza nae,” alisema Try Again.

“Yote haya yanayozungumzwa kwenye maeneo mbalimbali kuhusu hilo Pablo ndiye mwenye ukweli na uamuzi wa mwisho kama atabaki nasi Simba au ataondoka.”

SOMA NA HII  HITIMANA BANA...YANI BAADA YA KUICHAPA MTIBWA JANA...KAIFANANISHA KMC NA REAL MADRID ETI...