Home Habari za michezo KAMA KAWA..NABI KABAMBWA CHAMAZI AKIIPIGA CHABO SIMBA AISEE…ALIJIPIGA NGUO NYEUSI ASITAMBULIKE…

KAMA KAWA..NABI KABAMBWA CHAMAZI AKIIPIGA CHABO SIMBA AISEE…ALIJIPIGA NGUO NYEUSI ASITAMBULIKE…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameonekana kwenye uwanja wa Azam Complex kushuhudia mchezo wa ligi kati ya wenyeji Azam FC na Simba.

Nabi ameonekana akiwa ametupia nguo nyeusi na kofia nyeupe mashabiki wa chache wa Yanga waliojitokeza uwanjani hapo wameibua shangwe.

Uwepo wa Nabi kwenye mchezo huu umetafsiliwa kama amekuja kusoma mbinu za wapinzani wake kwenye kombe la Shirikisho la Azam hatua ya nusu fainali.

Wawili hao wanatarajia kukutana Mei 28 ukiwa ni mchezo wao wa nne msimu huu baada ya kukutana mechi mbili za ligi na kugawana pointi moja moja kwenye michezo yote miwili.

Mchezo wa tatu ulikuwa ni wa ngao ya Jamii Yanga akiibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Fiston Mayele.

SOMA NA HII  STAA MPYA WA AZAM ALIYESAJILIWA 'JUU KWA JUU' ...AFUNGUKA MAMBO YALIVYO KWA MABOSI HAO...KOCHA ATIA NENO...