Home Habari za michezo KAMERA ZA AZAM TV ZILIVYOMNASA NABI AKIWA ANAIPIGA SIMBA CHABO CHAMAZI JANA…

KAMERA ZA AZAM TV ZILIVYOMNASA NABI AKIWA ANAIPIGA SIMBA CHABO CHAMAZI JANA…


Kocha Mkuu wa Young Africans, Nasreddine Nabi jana Jumatano (Mei 18) alionekana kwenye uwanja wa Azam Complex kushuhudia mchezo wa ligi kati ya wenyeji Azam FC na Simba SC.

Nabi alionekana akiwa ametupia nguo nyeusi na kofia nyeupe, baada ya kunaswa na Kamera za Azam TV, iliyorusha moja kwa moja matangazo ya mchezo huo kutoka Azam Complex-Chamazi.

Uwepo wa Kocha huyo kutoka nchini Tunisia kwenye mchezo huo, umetafsiliwa kama sehemu ya kuanza kazi ya kuichunguza Simba SC kuelekea mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Miamba hiyo itakutana Jumamosi (Mei 28), Uwanja CCM Kirumba, ukiwa mchezo wa nne kwao tangu kuanza kwa msimu huu 2021/22.

Michezo mitatu iliyotangulia kwa miamba hiyo, miwli ilikua ya Ligi Kuu iliyomalizika kwa sare ya 0-0, huku mwingine ni ule wa Ngao ya Jamii uliomalizika kwa Young Africans ikiibuka ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Fiston Mayele.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSIKIA NAMUNGO WANAMTAKA...SIMBA WAMPANDISHA DARAJA MATOLA...