Home Habari za michezo KISA KUTOKUONDOKA NCHINI KAMA ALIVYOOMBA…KIGOGO SIMBA AMLIPUA MORRISON….ADAI SIMU HAPOKEI…AITAJA YANGA..

KISA KUTOKUONDOKA NCHINI KAMA ALIVYOOMBA…KIGOGO SIMBA AMLIPUA MORRISON….ADAI SIMU HAPOKEI…AITAJA YANGA..


Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu amemshangaa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison, kwa kushindwa kutimiza miadi waliyowekeana, baada ya klabu hiyo kumpumzisha hadi mwishoni mwa msimu huu.

Uongozi wa Simba SC mapema mwezi huu ulitangaza hadharani kumpa mapumziko Morrison hadi mwishoni mwa msimu huu, kufuatia matatizo yake binafsi, huku Mkataba wake ukielekea ukingoni.

Mangungu amesema Uongozi wa Simba SC ulikubaliana na Kiungo huyo mambo kadhaa, ili kumuwezesha kurudi nyumbani kwao Ghana kwa ajili ya kutatua matatizo yake, lakini cha kuchangaza Morrison alikatisha mawasiliano ghafla.

“Bernard Morrison aliomba kuondoka akashughulikie matatizo yake ya kifamilia, Sisi tulifanya kila kitu kuhusu safari yake ikiwa pamoja na kumkatia tiketi, Mpaka sasa hatujui alipo, simu hapokei, Kwa sababu Simba SC sio jela hatuwezi kuhangaika kumtafuta kujua alipo”

“Kama nyumbani kwao aliposema anakwenda ni Young Africans, basi atajua mwenyewe. Lakini viongozi wa klabu ya Young Africans watakuwa hawajitambui maana amewahangaisha sana” amesema Mangungu

Morrison anahusuishwa na mpango wa kusaini Young Africans, huku taarifa za baadhi ya vyombo vya habari zikidai tayari ameshamalizana na Uongozi wa klabu hiyo ili kukamilisha usajili wake huko Jangwani.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AANZA KUELEWEKA SIMBA....AFUNGUKA HILI KUHUSU 'SHOW' ZA NGOMA...