Home Habari za Simba KISA MAJERUHI YA LWANGA…KIUNGO MZAMBIA APEWA MKATABA SIMBA…PABLO ATOA MAELEKEZO MAZITO…

KISA MAJERUHI YA LWANGA…KIUNGO MZAMBIA APEWA MKATABA SIMBA…PABLO ATOA MAELEKEZO MAZITO…


UNAAMBIWA mwenendo wa majeraha kwa kiungo Taddeo Lwanga raia wa Uganda, umemfanya Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco alazimike kumuongeza mkataba mpya kiungo wake raia wa Zambia, Rally Bwalya.

Bwalya alisajiliwa Simba Agosti 15, 2020 akitokea Power Dynamos FC ya kwao Zambia, huku usajili wake ukizua taharuki kubwa kwa watani wao Yanga, ambapo tayari ameshaonyesha uwezo mkubwa ndani ya kikosi hicho jambo ambalo linamfanya Pablo kumuombea mkataba mpya.

Chanzo chetu kutoka Simba kimesema kwamba, pamoja na mkataba wa Bwalya kutarajiwa kuisha katikati ya msimu huu, majeraha ya Lwanga yameufanya uongozi huo kulazimika kumuongeza mkataba ili aweze kusaidiana na kiungo mkabaji atakayekuja kuchukua nafasi yake.

“Kuna wachezaji wengi wanatarajiwa kuachwa mwishoni mwa msimu huu na mmoja wapo ni Lwanga, ambaye hali yake ya afya imeshakuwa ya kutisha tangu alipofanyiwa upasuaji, hivyo uongozi umelazimika kumbakiza Bwalya ndani ya timu ili kulainisha safu hiyo ya kiungo.

Kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia Rally Bwalya yupo kwenye hatua ya kuongezewa mkataba na Simba kutokana na majeruhi ya Taddeo Lwanga anayetarajiwa kuachwa mwisho wa msimu

“Kocha ameutaka uongozi umpatie mkataba Bwalya kwa sababu bado anaamini kadri anavyopata michezo mingi atakuja kuwa mmoja wa viungo tishio nchini kwani ni kati ya wachezeshaji ambao wanaonekana wa kawaida kama usipoujua ufundi wake,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  WALIOFUNGWA GOLI 7 BILA WAIPA YANGA MBINU ZA KUIFUNGA CLUB AFRICAIN KESHO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here