Home Habari za michezo KISA MATOKEO YA SARE YANGA…ZAHERA NAYE KASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA KINACHOIMALIZA YANGA….

KISA MATOKEO YA SARE YANGA…ZAHERA NAYE KASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA KINACHOIMALIZA YANGA….


KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwamba timu hiyo bado ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa, lakini akatoa mbinu na angalizo kwa mashabiki na wachezaji.

Alichosema Zahera ambaye hivi karibuni anarudi kuifudisha timu ya taifa ya DR Congo, ni kwamba wachezaji wa Yanga wamejiweka katika mazingira magumu ya kucheza kwa presha bila sababu ya msingi hali ya kuwa anajua matajiri wao GSM na makocha wao wamefanya karibu kila kitu. 

“Ni presha tu ndio kitu unaona kimewakumba wachezaji hakuna kingine, wanakila kitu wamepata kutoka kwa makocha na uongozi wao,” alisema Zahera na kuwataka mashabiki kuacha kuwapa persha wachezaji. “Wachezaji walizoea kushinda hali hiyo wanapokosa kufunga mechi tatu wanapata presha kubwa,wanajishangaa ile inatakiwa ifanyike kazi ya kuondoa hiyo hali. Unaona lile soka la Yanga limerudi timu inacheza inasogea juu inazuia, hakuna kitu hatarishi ambacho Prisons walifanya. 

Yanga ilitengeneza nafasi nyingi bora za kufunga lakini hawakuwa na akili ya kutulia kumalizia, hapo huwezi kusema makocha hawakufanya kazi yao,” alisema Zahera na kuwataka wachezaji ubinafsi na kuitanguliza timu kwanza katika kutumia nafasi wanazotengeneza kwenye mechi zao akitolea mfano makosa ya kiungo Feisal Salum.

“Feisal hakuwa na sababu ya kutaka kumpa Mayele kufunga ukiangalia vizuri hata Mayele alidhani Feisal atafunga mwenyewe lakini hakufanya kibaya ila alitakiwa kumalizia mwenyewe.

“Ni kitu bora Mayele akiwa mfungaji bora ile inaonyesha wachezaji wanataka mafanikio ila kitu bora ni kuitanguliza timu kama wangepata bao pale ukizingatia walitoka kutokupata bao mechi mbili nyuma, mabao zaidi yangepatikana.

“Hata ile penalti nilidhani angepiga Djuma kwa kuwa alikwenda na alikuwa ameshafunga.”

SOMA NA HII  CAF YAWAOKOA YANGA SAKATA LA USAJILI WA MORRISON...ATUMIWA RATIBA YOTE KWAO GHANA...MSUVA AWEKWA KANDO...