Home Habari za michezo KISA SIMBA KUPIGWA FAINI NA CAF….MANARA ATAKA KUJIUA…ADAI NCHI IMEAIBISHWA…MASHABIKI WASHUKA NAYE...

KISA SIMBA KUPIGWA FAINI NA CAF….MANARA ATAKA KUJIUA…ADAI NCHI IMEAIBISHWA…MASHABIKI WASHUKA NAYE MAZIMA…


Ikiwa ni saa chache baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuiadhibu Klabu ya Simba kwa kuipiga faini ya Tsh milioni 23 kwa kosa la kufanya tambiko hatarishi ndani ya uwanja wakati wa mechi yao ya marejeano ya robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates, Msemaji wa Yanga, Haji Manara aliibuka na waraka mzito.

Manara aliandika haya: “Wakati Watanzania tunaendelea kutangaza Filamu kubwa ya Royal Tour kuna wenzetu leo wamepigwa faini ya Dola Elfu kumi kwa kufanya Matambiko Hatarishi ugenini.

“Yaan Sisi tukitangaza Nchi yetu Kwa Vivutio vyake, Wenzetu wengine Kwa Maksudi wameenda kuiambia Dunia,,Sisi ni Wanga na Wachawi.

“Nchi imefedheheshwa,,Watanzania Tumedhalilishwa na Mpira wetu tumeutia doa, kama Senior Citizen wa Taifa hili nimejisikia kinyaa Kwa aibu hii kubwa zaidi kuwahi kutokea katika Taifa letu. ,,halaf huo Ulozi wenu mliufanya ndani ya Mwezi wa Ramadhani,,Daaah sijui nife tu ,,maana aibu hii haivumiliki kwa kweli

“Ipo haja ya Watanzania kuombwa Radhi kwa hii fedheha tuliyoipata leo, Vinginevyo wanapaswa pia kupewa adhabu ya ndani ikiwemo kufungiwa miaka kumi kuwakilisha Nchi…

“Lazma Tanzania ichukue hatua sahihi za ndani ili aibu hii isirudie tena, Kesho nasafiri kwenda Ulaya itabidi nihairishe,,maana huko Airport za wenzetu nikitoa Passport tu, watajua na mimi Mwanga .Yaan Mnaenda kuwanga huku Dunia inaona?”

Baada ya kauli hiyo, Mashabiki wakamiminika;

officialjackilin; Ukimaliza uposti ile ya kufukia hirizi kwa mkapa mbuzi wa kafara wewe.

ra.madhani5089; Acha wivu ww mbona nyiee mmelogaa taifa Juma Shabani mmetumaa mulikua mnafanyajee paleee unajifanya mwemaa, Sana angalia yako fika na ww robo final acha wivu mzeee eti tuchukuliwe atua juma shabani kafanya wanga Waz Waz kwa mkapaa zidi ya Ruvu Shooting nini kuleee boys wewe.

SOMA NA HII  KWA HIKI KITASA KIPYA CHA YANGA...MASTRAIKA LIGI KUU WATAFUTE PA KUPITA....JAMAA NI RAMOS MTUPU......

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here