Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….MAYELE AFUNGUKA ATAKACHOWAFANYA SIMBA…”LAZIMA TIMU MOJA IPITE”…

KUELEKEA MECHI YA KESHO….MAYELE AFUNGUKA ATAKACHOWAFANYA SIMBA…”LAZIMA TIMU MOJA IPITE”…


Mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Fiston Mayele, amesema kuwa ili wafanikiwe kubeba makombe yote mawili yaliyobaki, ni lazima wawafunge watani wao, Simba.

Yanga na Simba zinatarajiwa kuvaana keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ukiwa ni mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mayele alisema katika mchezo huo, wanahitajika kupata ushindi utakaowawezesha kuvuka na kwenda fainali.

Mayele alisema wanafahamu majukumu waliyonayo ambayo ni lazima wapate ushindi ili kufikia malengo ya kuchukua makombe mawili ikiwemo Ligi Kuu Bara na michuano hiyo.

Aliongeza kuwa, maandalizi waliyoyafanya yanatosha kupata ushindi ili kufanikisha malengo waliyonayo.

“Malengo yetu kabla ya kuanza msimu huu yalikuwa ni kubeba makombe yote tunayoshindania.

“Kwa hatua hii tuliyofikia ni lazima timu moja ipate ushindi ili ifuzu kucheza fainali kati yetu dhidi ya Simba.

“Kama wachezaji tumepanga kupata ushindi katika mchezo huu ili tucheze fainali na kuchukua ubingwa, kama tumetoka sare katika ligi, basi safari hii hatutawaacha,” alisema Mayele.

Katika Ligi Kuu Bara ambapo Yanga inaongoza ikiiacha Simba kwa pointi 14, vinara hao wanahitaji pointi tatu kwenye mechi nne zilizobaki kufikisha 67 ili kuwa mabingwa.

SOMA NA HII  A-Z 6G ZA SIMBA ZILIVYOWATAPISHA NYONGO JWANENG.....CHAMA AACHA MSHANGAO TAIFA...