Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA LEO….DODOMA JIJI WAMWANDALIA MAYELE ‘KAZI CHAFU’ …WACHEZAJI WALA KIAPO…

KUELEKEA MECHI YA LEO….DODOMA JIJI WAMWANDALIA MAYELE ‘KAZI CHAFU’ …WACHEZAJI WALA KIAPO…


Kocha Msaidizi wa Kikosi cha Dodoma Jiji Mohammed Muya amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Yanga huku akidai wamejipanga kuhakikisha mshambuliji wa Yanga Fiston Mayele hatetemi.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi kuu ikiwa na alama 28 huku vinara Yanga wakiwa kileleni na pointi 57.

Kocha huyo amesema: “Hiyo kutetema kwetu hatuifikirii kabisa nimekwambia sisi niwahitaji kutetema hakupo kesho ‘leo’,”

Amesema morali ya wachezaji ipo juu na michezo yao mitatu ya mwisho wamepata alama saba wakishinda dhidi ya Biashara, Mbeya City na kutoka suluhu dhidi ya Polisi Tanzania ugenini.

“Kama mwalimu unajua kinachotakiwa kwa wachezaji wako hakuna cha kuogopa timu yoyote, vigezo vya kuwa washindani tunavyo tunawaita mashabiki wetu waje.

Mchezaji wa timu hiyo,Omary Kanyoro amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

SOMA NA HII  MBRAZILI ATOA AHADI YA KIBABE SIMBA....MASHABIKI WAPAGAWA KINOMA...