Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO….SIMBA KUSHUSHA ‘KIFAA HIKI CHA KINIGERIA’….ANAKIPIGA LIGI YA URENO…ISHU IKO...

KUELEKEA MSIMU UJAO….SIMBA KUSHUSHA ‘KIFAA HIKI CHA KINIGERIA’….ANAKIPIGA LIGI YA URENO…ISHU IKO HIVI…


MAJERAHA ya muda mrefu aliyokumbana nayo kiungo wa Simba, Taddeo Lwanga raia wa Uganda, yamewafanya mabosi wa klabu hiyo kukata jina lake na kumtafuta mbadala wake ambaye ni Oche Ochowechi kutoka Nigeria.

Ochowechi ambaye aliwahi kuja hapa nchini na kikosi cha Plateau United kilichocheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita dhidi ya Simba, kwa sasa anaitumikia CD Feirense inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Ureno aliyojiunga nayo Septemba 1, 2021.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimesema kuwa, tayari mabosi wa timu hiyo wameshakamilisha mazungumzo na Ochowechi na kwamba atatua hapa nchini mara tu baada ya msimu huu kumalizika ili kuwahi kambi ya kujiandaa na msimu ujao.

“Tumshukuru Mungu sana sisi kama Simba tayari tumeshapata mbadala wa Lwanga, ni yule kiungo Mnigeria, Ochowechi ambaye aliwahi kuja hapa nchini na Plateau United, muda wowote atatua hapa nchini kuungana na timu yetu.

“Uongozi umeamua kuachana na Lwanga kutokana na kuwa na majeraha ambayo yalimfanya kukaa nje kwa muda mrefu kiasi kwamba hata akirejea uwanjani, hatakuwa kama alivyokuwa awali,” kilisema chanzo hicho.

Ikumbukwe kuwa, Lwanga alijiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Tanta SC ya Misri.

SOMA NA HII  PAMOJA NA TIMU KUWA 'HOI' UWANJANI...AZAM FC WAKANA MPANGO WA KUACHANA NA LWANDAMINA...