Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO….YANGA WAPANGA KUTIKISA AFRIKA KWA USAJILI…INJINIA HERSI ATAJA VIFAA VIPYA...

KUELEKEA MSIMU UJAO….YANGA WAPANGA KUTIKISA AFRIKA KWA USAJILI…INJINIA HERSI ATAJA VIFAA VIPYA TUPU…


MJUMBE wa Kamati ya Mashindano na Usajili wa Yanga ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, ameahidi msimu ujao kufanya usajili mkubwa zaidi utakaokuwa gumzo Afrika kwa kushusha mashine hatari zaidi ya Khalid Aucho na Yannick Bangala.

Hiyo ni baada ya msimu huu unaoelekea ukingoni kushusha vifaa vya maana wakiwemo nyota hao wanaoibeba timu hiyo. Wengine ni Djuma Shaban, Fiston Mayele, Djigui Diarra na Salum Aboubakari ‘Sure Boy’.

Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Yanga kuelekea msimu ujao ni kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas, Aziz Ki na Bernard Morrison ambaye mkataba wake Simba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Hersi alisema kikubwa walichopanga katika usajili wa msimu ujao ni kuhakikisha wanafanya usajili wenye faida utakaowawezesha kufikia malengo ya kufika mbali katika michuano ya kimataifa.

Aliongeza kuwa, wamepanga kuwatumia baadhi ya mawakala wa kimataifa katika kuwapata wachezaji wa daraja la juu baada ya kuifanyia kazi ripoti ya Kocha Nasreddine Nabi atakayoikabidhi kwa uongozi.

“Malengo yote katika timu ni kuifanya Yanga inakuwa bora kwa kuwaleta wachezaji wa daraja la juu kabisa katika kila msimu na hilo linawezekana kwetu kutokana na malengo yaliyokuwepo.

“Ili tuwe bora ni lazima kila usajili tukiboreshe kikosi chetu kwa kuwaleta wachezaji wa viwango vya juu kabisa, utaona mwanzoni mwa msimu tulifanya usajili bora ambao ulisifiwa na kila shabiki wa Yanga.

“Katika dirisha dogo, tulipokea mapendekezo ya kocha akiomba tumsajili kipa, tukamleta Mshery (Aboutwalib) ambaye ameonesha kiwango bora. Pia akapendekeza tumsajili kiungo, tukamleta Sure Boy ambaye yeye ameonesha ubora wake na kuingia katika kikosi cha kwanza.

“Hicho ndicho tutakachokifanya katika kuelekea msimu ujao, tumepanga kufanya usajili bora kwa kuwaleta wachezaji wa daraja la juu zaidi ha hawa tuliokuwa nao msimu huu,”alisema Hersi.

SOMA NA HII  WAKATI HATA UHAKIKA WA KUPATA NAFASI HAUPO...NKANE AIBUKA NA HAYA MAPYA KWA YANGA...'AJIPALILIA MOTO JIKONI'...