Home Habari za michezo KUHUSU ALIPO DEO KANDA NA KWA NINI HATUMINI…MTIBWA SUGAR WAVUNJA UKIMYA…WAITAJA TFF…

KUHUSU ALIPO DEO KANDA NA KWA NINI HATUMINI…MTIBWA SUGAR WAVUNJA UKIMYA…WAITAJA TFF…


Uongozi wa Mtibwa Sugar unaendelea kupambana ili kupata vibali vitakavyomuwezesha Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Deo Kanda kujumuika na wachezaji wenzake, katika michezo iliyosalia msimu huu 2021/22.

Mkuu wa Idara ya Habari na mawasilino ya Mtibwa Sugar Thobis Kifaru amezungumza na Dar24 Media na kueleza mkakati waliojiandaa nao, ili kufanikisha kiungo huyo anaonekana dimbani.

Kifaru amesema mwanasheria wa Mtibwa Sugar anashughulikia suala la Kanda kwa kufuatilia ndani ya Shirikisho la soka nchini TFF, ambalo lina mamlaka ya kumuidhinisha mchezaji kucheza ama kutokucheza Ligi za ndani.

“Kanda yupo Dar es salaam sambamba na mwanasheria wa Mtibwa Sugar, wanafuatilia suala la vibali TFF, tunaamini mambo yatakwenda vizuri na ataanza kuonekana akiwa na kikosi chetu kabla ya msimu huu kumalizika.”

“Tumeona Mwanasheria wetu ni bora akaenda TFF ili kulijadili suala la Deo Kanda, ili lipatiwe ufumbuzi kwa sababu limechukua muda mrefu sana.”

“Mchezaji huyo anajua majukumu yake, tangu alipojiunga nasi amekua na jambo kubwa analionyesha katika mazoezi yetu, ana nidhamu kubwa sana na ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuisaidia Mtibwa Sugar.”

“Naamini suala lake likikamilishwa na akaanza kucheza kwenye kikosi cha Mtibwa Sugar, tutaona kitu kikubwa sana kutoka kwake, sisi kama uongozi tunaendelea kupambana ili kumsaidia afikie malengo yake.” amesema Kifaru

Kwa mara ya kwanza Deo Kanda alicheza Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na Mabingwa watetezi Simba SC kabla ya kurejea nchini kwao DR Congo kwenye klabu iliyomtoa kwa mkopo TP Mazembe.

SOMA NA HII  YANGA WAMUIBUA KOCHA TABORA UNITED..... JAMBO LAFIKA TFF ISHU NZIMA IKO HIVI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here