Home Habari za michezo KUHUSU UBINGWA MSIMU HUU….NABI ARUDISHA AMANI YANGA…AJIPA JUKUMU LA KUFANYA ‘MIUJIZA’…

KUHUSU UBINGWA MSIMU HUU….NABI ARUDISHA AMANI YANGA…AJIPA JUKUMU LA KUFANYA ‘MIUJIZA’…

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo, kwa kuwaambia: “Mashabiki acheni presha, niachieni mimi, ninajua kitu cha kufanya kitachotupa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.”

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya wapinzani wao Simba walio nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 kupata matumaini ya kutetea ubingwa kufuatia Yanga kupata suluhu tatu mfululizo.

Yanga ilianza kupata suluhu dhidi ya Simba, zikafuatia nyingine mbili dhidi ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons.

Nabi alisema kuwa ameshajua tatizo lililopo katika timu yake ambalo lilisababisha wapate suluhu kwenye michezo mitatu mfululizo ya ligi.

Nabi alisema kuwa mashabiki waondoe hofu juu ya ubingwa, kwani hautakwenda popote kutokana na mikakati mipya atakayokuja nayo kwa kuanzia mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Aliongeza kuwa tayari amefanya kikao na wachezaji wote juzi Jumanne jioni mara baada ya kikosi hicho kuingia kambini kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Mimi sina hofu juu ya ubingwa, lakini hofu kubwa ni kwa mashabiki ambao wameipata baada ya matokeo matatu ya mfululizo ya suluhu ambayo tumeyapata.

“Mashabiki waondoe hofu, kwani ninajua kitu cha kukifanya hivyo waniachie mimi na wasubirie sapraizi kutoka kwangu.

“Nafahamu matokeo yamewaumiza, lakini kikubwa wasiwaseme sana wachezaji wangu na badala yake kuwapa morali ya kupambana ili kufanikisha malengo yetu katika michezo ijayo ya ligi,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  KUEPUSHA AIBU KESHO....MGUNDA AHAIDI 'KUNG'ATA MENO' DHIDI YA WAMALAWI...TSHABALALA ATAJA 'UCHAWI'....