Home Habari za michezo KUHUSU UBINGWA WA MSIMU HUU…SIMBA WAISHUTUMU YANGA KWA PROPAGANDA …MORRISON ATAJWA…

KUHUSU UBINGWA WA MSIMU HUU…SIMBA WAISHUTUMU YANGA KWA PROPAGANDA …MORRISON ATAJWA…


Vita ya kuwania Taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, imeendelea kupamba moto kati ya Simba SC na Young Africans huku alama 08 zikizitofautisha klabu hizo katika msimamo.

Simba SC inayotetea Taji hilo kwa mara ya tano ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 49, huku Young Africans inayolisaka Taji la Ligi Kuu kwa msimu wa tano mfululizo ikiwa kileleni kwa kufikisha alama 57.

Simba SC wanaamini tetesi za usajili wa Bernard Morrison kwenda Young Africans zinazoendelea katika mitandao ya kijamii ni sehemu ya Propaganda za vita ya kuwania Ubingwa msimu huu.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amethibitisha kushtukiwa kwa Propaganda hizo zinazotumiwa na Upande wa pili, huku akisistiza kuwa klabu yao haitoyumbishwa na Popaganda hizo.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa ufafanuzi wa Proganda hizo kwa kuandika: Mmeanza cheap propaganda kuhusu wachezaji wetu

SOMA NA HII  MOSES PHIRI AFUNGUKA SABABU YA KUICHINJA YANGA NA KUTUA SIMBA...ADAI HANA MPANGO KUWA MCHEZAJI BORA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here