Home Habari za michezo MAMBO TAYARI HUKOO JAMENI….MKUDE,LWANGA, MORRISON NA TADEO LWANGA ‘OUT’ SIMBA….

MAMBO TAYARI HUKOO JAMENI….MKUDE,LWANGA, MORRISON NA TADEO LWANGA ‘OUT’ SIMBA….


Viungo wanne wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo Jumatano (Mei 11) wataukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, utakaounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa mishale ya saa moja usiku.

Mchezo huo ni wa Mzunguko wa Pili baada ya ule wa Mzunguko wa kwanza Kagera Sugar kuwatungua bao 1-0 Simba SC, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Kocha Mkuu wa Simba SC Pablo Franco Martin amethibitisha kuwakosa wachezaji Jonas Mkude, Bernard Morrison, Sadio Kanoute na Taddeo Lwanga.

“Mkude,(Jonas),Morrison,(Bernard),Kanoute,(Sadio) na Lwanga,(Taddeo) hawa wataukosa mchezo kwa kuwa bado hawajawa fiti na ni majeruhi.

“Lakini kuwakosa hawa haina maana kwamba hawatakuwepo wengine, wapo wachezaji ambao tumewaandaa kwa ajili ya mchezo wetu huo muhimu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kushuhudia mchezo wetu muhimu na tunaamini kwamba ushindani utakuwa mkubwa lakini tupo tayari,” amesema Kocha Pablo.

Simba SC inashuka Dimba SC ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Barakwa kufikisha alama 46, huku Kagera Sugar iliyopoteza mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold kwa kufungwa 1-0 ipo nafasi ya 7 kwa kufikisha alama 29.

SOMA NA HII  REFA MECHI YA SIMBA SC VS HOROYA AC...KAMA YUPO FEA FEA VILEE...MNYAMA ASHINDWE YEYE KWA MKAPA