Home Burudani MIAKA 5 TOKA WATUE BONGO…SportPesa NI BABA LAO…MZIGO WA JACKPOT WAZIDI KUNONA…WALIPA...

MIAKA 5 TOKA WATUE BONGO…SportPesa NI BABA LAO…MZIGO WA JACKPOT WAZIDI KUNONA…WALIPA Tsh BIL 63.3..


KATIKA kipindi cha miaka mitano ya Kampuni ya SportPesa Tanzania kuwapo hapa nchini wamechangia pato la taifa kwa kulipa kodi kwa serikali kiasi cha Sh. bilioni 434.7 (majumuisho ya kodi zote), huku washindi waliopatikana kutokana na kubashiri kwa ufasaha wakiwa wamelipwa jumla ya Sh. bilioni 
63.3, anaeleza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Tarimba Abass, katika makala haya maalum.

Tarimba alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati akielezea mafanikio ya kampuni hiyo ndani ya miaka mitano tangu kuanza shughuli zake nchini Mei 09, 2017.

Tarimba, alisema kuzaliwa kwa SportPesa ni baada ya kuona fursa ya kuwasaidia Watanzania kuwainua kiuchumi na kuipatia serikali mapato makubwa sambasamba na kupata faida na kuwa tayari kushindana na washindani wengine kiweledi na si kijanjajanja ili Watanzania waweze kuiona kampuni hiyo kuwa ni bora na inafaa.

“Uwapo wetu Tanzania uziondoa zile kodi nyingine za PAYE na vile vidogodogo, sisi tumeshailipa serikali shilingi bilioni 434.7, ni fedha nyingi, watu wasituone ni watu wa mchezo wa kubahatisha, wengine wanatutania wanatuita watu wa kamari, tunafanya mchango mkubwa pengine kuliko viwanda vingi na sidhani kama kuna mfanyabiashara anaweza kulipa fedha nyingi kama hizi,” alisema Tarimba.

Aliongeza kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imetoa zawadi za mbalimbali zenye thamani ya Sh. bilioni 344.4.

“Zawadi ambazo tumewalipa Watanzania tangu tumeanza Mei 2017 mpaka leo ni Sh. bilioni 344.4, hivyo naweza kusema tumetekeleza ile azma yetu, tutawasaidia Watanzania kuwainua kichumi na humu ndani tumeshatoa Jackpot mara sita zenye thamani tofauti tofauti.

“Kuna watu wamepata milioni 200 wengine 300, nyingine nakwenda mwenyewe nawaona, familia za watu masikini zinabadilika kuwa za uchumi wa kati na kuendelea kwa kufanyabiashara kwa kutumia fedha walizoshinda SportPesa,” alisema.

Tarimba anasema kuwa zawadi kubwa ambayo SportPesa imewahi kuitoa ndani ya miaka mitano ni Sh. milioni 800 ambayo walishinda vijana wawili mmoja akifanya kazi Jeshi la Magereza na mwingine Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao waligawana milioni 400 kila mmoja.

“Hawa watu naweza kusema kuwa wanajumuika na wengine waliopata milioni 20, 30 na milioni 40 hao ni wengi sana, hii tunakwenda kuwawezesha na wao pia wamelipa kodi serikalini kupitia zawadi wanazopata,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema SportPesa ni kampuni pekee kwa sasa ambayo inayo Jackpot ya Sh. bilioni 1.2 ipo inasubiri mtu kushinda. “Niambie Mtanzania akipata pesa kama hiyo umemtoa katika hatua gani, umempeleka hatua gani? Alihoji Tarimba.

Tarimba ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Bahati Nasibu ya Taifa enzi hizo, alisema kuwa ‘betting’ ni mchezo wa burudani, na mchezo wenye uelewa ndio maana unaitwa ‘skill game’ kwa kuwa ni mchezo ambao unachezwa na watu wenye uelewa na uzoefu.

“Hii si pata potea kwamba uchukue namba 1, 2, 3 useme kwamba mimi najaribu namba 3 hapana, wachezaji wote wa ‘betting’ hata kama watu wanawatania kwamba wanacheza watu wasio na kazi, naweza kusema ni uchache wa uelewa, hata wale wanaowasema wachezaji wa ‘betting’ kwamba wanajazana kwenye vibanda wanasahau faida wanazozileta kwenye nchi hii kwa kulipa kodi,” alisema Tarimba na kuongeza kuwa;

“Mojawapo ya faida ni kodi zinazolipwa, uwapo wa hawa watu kwenye vibanda ambavyo vimesajiliwa, na wakacheza wanachangia vilivyo pato la taifa, hiyo nazungumzia tu SportPesa kwa miaka mitano, je, kwa makampuni mengine katika kipindi cha miaka mitano, tumeingiza kiasi gani?” Alihoji Tarimba.

SOMA NA HII  KUEPUSHA AIBU KESHO....MGUNDA AHAIDI 'KUNG'ATA MENO' DHIDI YA WAMALAWI...TSHABALALA ATAJA 'UCHAWI'....

Alisisitiza kuwa anatamani siku moja kufanyike mdahalo kuhusiana na michezo ya ‘betting’ ili watu waone na kufunguka macho, kwamba michezo ya kubahatisha hasa ‘betting’ ni michezo yenye faida kubwa kwa taifa hili.

Tarimba ambaye ni Mbunge wa Kinondoni, alisema kuwa kwa mfano kwa mwaka 2021 kodi ya wanaocheza na kupata zawadi walikuwa wanalipa asilimia 20 serikalini, akipata milioni 100, milioni 20 inakwenda serikalini.

Alifafanua kuwa “serikali ilipunguza asilimia tano, sasa kupunguza kwake ilikuwa ni nini, kwamba kuna watu sasa hivi wanacheza ‘betting’ kwenye kampuni za nje ambazo hazilipi kodi nchini, taifa halipati faida.

“Kinachowapeleka kucheza kwenye kampuni za nje ni kwa sababu hawalipi kodi, serikali ikashauriwa embu punguzeni hapo ili kuona itasaidia watu kucheza zaidi Tanzania.

“Hatima yake ilivyoondolewa asilimia tano na sasa watu wakawa wanalipa asilimia 15, ikaongeza thamani ya watu wanaocheza na fedha ambazo zimekuja serikalini kutoka Julai 2020 hadi Desemba ilikuwa bilioni 10.6 baada ya mabadiliko serikali kuondoa asilimia tano mwaka 2021 serikali imepata kodi bilioni 14.”

Alisema kumbe kwenye nchi kama ukipunguza kodi, unachochea matumizi zaidi na hivyo unasababisha serikali ipate zaidi, na kwamba watu walikuwa na hofu endapo serikali ikipunguza itapata hasara jambo ambalo si la kweli.

Tarimba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, alisema katika kipindi cha miezi sita wachezaji walilipa kodi ya Sh. bilioni 27 inayotokana na zawadi, jambo ambalo linaonyesha michezo hii kama itakuwa inasikilizwa vizuri na wafanya inaweza kusaidia kuinua pato la taifa.

“Katika mwaka 2021-2022 serikali ilikuwa imepanga ipate bilioni 150 kwenye mwaka wa fedha ambao unamalizika keshokutwa, hivi ninavyozungumza makusanyo yapo asilimia 90 na zaidi, hivyo serikali inakwenda kufikia malengo yake,” alisema Tarimba.

Akizungumzia mipango ya kampuni hiyo kwa miaka mitano ijayo, Tarimba alisema ni kuhakikisha mafanikio ambayo yamepatikana tangu kuanzishwa SportPesa yanaongezeka na kuwa kampuni inayoongoza kama ilivyo sasa kwenye kampuni za kubashari.

“Hatuna sababu ya kukaa nyuma, kwa sababu tuna weledi wa kutosha, kwa mfano wafanyakazi wetu nikiwamo mimi pia tunauzoefu mkubwa sana katika uendeshaji wa michezo hii si biashara, masuala ya kisheria, masuala ya kimifumo na teknolojia… tunauzoefu mkubwa sana, kibiashara tunavyokubalika sasa tungependa kuona tuwe maradufu,” alisema na kuongeza kuwa;

“Sisi madhumuni yetu ni kutanuka kutoka asilimia 30 ya ‘marketing share’ na kufikia asilimia 40 hadi 50 na hiyo ina hakisi kwamba tungependa kukubalika na Watanzania, yaani mtu akifikiria kubetting Tanzania aifikirie SportPesa,” alisema.

Aidha, alisema kampuni hiyo imeajiri Watanzania zaidi ya 104, na katika miaka mitano ijayo wanatarajia kuongeza zaidi ajira pamoja na kuongeza thamani ya zawadi kwa wachezaji.

“Kwa mfano hii bilioni 1.2 ya Jackpot ikishaliwa, tunampango wa kuitambulisha Jackpot nyingine yaani tuwe nazo mbili.

kumbukwe kuwa Jackpot hii ilianza kwa Sh. milioni 200, lakini imewekezwa hadi kufika bilioni 1.2 sasa tunataka kuja na Jackpot mpya baada ya hii kuliwa, tunampango kuwa na Jackpot ya milioni 200, pia tuna Jackpot ambayo itaanza kwenye bilioni 1 hii ndio muelekeo wetu wa kutoa zawadi zaidi na kuwafanya Watanzania kupata fedha zaidi kutoka katika shughuli zetu,” alisema Tarimba.

Credit : Nipashe.