Home Habari za michezo NI MWAKALEBELA TENA…AIBUKA NA HAYA MENGINE KUHUSU MAYELE…NI BAADA YA KUKOSA PENATI...

NI MWAKALEBELA TENA…AIBUKA NA HAYA MENGINE KUHUSU MAYELE…NI BAADA YA KUKOSA PENATI JUZI…


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, ameweka wazi kuwa licha ya kupoteza mkwaju wa penati katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Jumatatu iliyopita, straika wao, Fiston Mayele hana presha yoyote na amejipanga kuwanyamazisha wakosoaji wake kwa kufunga mabao mengi zaidi kwenye michezo ijayo.

Jumatatu wiki hii Yanga wakiwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam walilazimishwa suluhu dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, huku tukio la Mayele kukosa penalti likizua mjadala mkubwa.

Suluhu hiyo ilikuwa ni ya tatu mfululizo kwa Yanga ambayo imewafanya wafikishe pointi 57 na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kucheza michezo 23.

Mwakalebela alisema: “Kwanza kabisa niwatoe hofu mashabiki wetu kuwa hali ni shwari na hakuna changamoto yoyote kwenye kikosi kwa sasa, ni kweli hatujawa na matokeo mazuri katika michezo yetu mitatu iliyopita lakini tunaendelea kupambana kufanikisha malengo yetu.

“Ishu ya kukosa penalti inaweza kutokea kwa mchezaji yeyote na wala hakuna presha yoyote iliyowekwa kwa Mayele kwa sasa, zaidi sana amejipanga vizuri kuendeleza moto wake wa kufunga mabao na kuwanyamazisha wale wote ambao wanamkosoa kwa sasa.”

SOMA NA HII  LEO NI USIKU WA UEFA...KWA MTONYO KIDOGO TU ODDS ZA MERIDIANBET ZINAKUPA UHAKIKA WA MAISHA...