Home Habari za michezo RASMI…YANGA WATANGAZA KUACHANA NA SAIDO NTIBAZONKIZA…..KUPISHANA NA MORRISON SIMBA….

RASMI…YANGA WATANGAZA KUACHANA NA SAIDO NTIBAZONKIZA…..KUPISHANA NA MORRISON SIMBA….


Uongozi wa Yanga SC umetangaza kumalizana na Mchezaji Saidi Ntibazonkiza huku taarifa hiyo ikisema Mchezaji huyo amemaliza mkataba wake wa miaka miwili.

Taarifa ya Yanga imesema “Uongozi unapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mchezaji wetu Saidi Ntibazonkiza kwa utumishi wake ndani ya Yanga SC, tunamtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha yake ya soka nje ya klabu ya Yanga”

Katika siku za hivi karibuni Saido amekuwa akituhumiwa kutosaini mkataba aliopewa na mabosi wa Yanga kwa kile kilichodaiwa kusikilizia ofa ya Simba, ambao awali walionyesha kumuhitaji na kuanza mazungumzo yake.

Hata hivyo, Yanga waligundua hilo na kumpa mkataba mapema , ambao alikuwa akiwazungusha katika kuusaini, mpaka alipofukuzwa kambini kwa kile kilichodai kuandaa mpango wa kuhujumu timu kuelekea mechi dhidi ya Simba kwenye nusu fainali ya kombe la shirikisho la Azam.

Wakati wa mkataba wake na Yanga, Saido atakumbukwa kwa kiwango bora alichokionyesha huku magoli yake ya kiufundi yakimpatia umaarufu zaidi miongoni mwa mashabiki wa Yanga na soka la bongo kwa ujumla.

Mbali na Yanga, Saido pia amepita timu mbalimbai za Afrika na Ulaya, ambapo pia alipata bahati ya kucheza Ligi Kuu ya Ufaransa, hivi sasa staa huyo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Burundi.

SOMA NA HII  KOCHA AZAM FC AITEMEA CHECHE SIMBA SC....APANIA KUMTIBULIA JAMBO MGUNDA...