Home Habari za michezo RONALDO AKIWA NDANI…’MAN UTD WAZIDI KUGAWA URODA’ EPL….BRIGHTON NAO ‘WAJICHOVYEA ASALI’..

RONALDO AKIWA NDANI…’MAN UTD WAZIDI KUGAWA URODA’ EPL….BRIGHTON NAO ‘WAJICHOVYEA ASALI’..


Timu ya Manchester United imeendelea kukubali vichapo vya aibu baada ya kubamizwa na Brighton and Hove Albion kipigo cha bao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

Mabao ya Brighton yamefungwa na Cuicedo dakika ya 15, Cucurella dakika ya 49, GroB dakika ya 57 na Trossard dakika ya 60 huku Ronaldo akishindwa kutamba kabisa.

Man United ambao wamekuwa wakisuasua na kupokea vichapo vya kutosha licha ya ukubwa wao duniani kwa sasa wapo nafasi ya sita ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

Vipigo vingine ambavyo Man United wamevipokea msimu huu ni.

Brighton 4-0 Man United Man United 0-5 Liverpool Liverpool 4-0 Man United Watford 4-1 Man United Man City 4-1 Man United Leicester 4-2 Man United Arsenal 3-1 Man United.

SOMA NA HII  BARBARA ATOBOA SIRI...USAJILI WA ADEBAYO KUTUA SIMBA