Home Habari za michezo WAKATI MATANGAZO YAKIWA ‘LIVE’… BBC WAIITA MAN UTD TAKATAKA…CEO WAO AFICHUA ALIYEFANYA...

WAKATI MATANGAZO YAKIWA ‘LIVE’… BBC WAIITA MAN UTD TAKATAKA…CEO WAO AFICHUA ALIYEFANYA MCHEZO HUO…


Shirika la utangazaji nchini Uingereza BBC limeiomba radhi klabu ya Manchester United baada ya maneno ya kuikashifu klabu hiyo kuoneka kwenye matamgazo yao ambayo yalisomeka ‘Manchester United are rubbish’.ikiwa na maana kwa tafsiri isiyo rasmi kuwa ‘Manchester United ni takataka’

BBC wameeleza kuwa bahati mbaya hiyo imefanywa na mfanyakazi ambaye alikuwa anajifunza jinsi ya kurusha jumbe za maandishi za matangazo, halikuwa jambo walilodhamiria.

“Mapema leo, baadhi yenu mmeweza kuona kitu kidogo cha tofauti kwenye matangazo yetu ya maandishi chini ya screen ya matangazo ya habari, ambao uliandikwa kuhusu Manchester United, alisema mteangazi wa BBC.

“Natumai kwamba haikuwa kuwashutumu mashabiki wa Manchester United, Ngoja niwaelezee nini kilichotokea.

“Nyuma ya pazia, kuna mtu alikuwa anajifunza jinsi ya kuweka jumbe za matangazo ya maandishi, kwaiyo alikuwa anaandika tu pasipo mpangilio.

“Ndio jumbe hiyo ikaonekana kwaiyo tunaomba radhi kama umeona hilo na kuhisi umeonewa na kwa mashabiki wa manchester United lakini hakika ilikuwa ni makosa na haikupaswa kuonekana kwenye screen.

“Hivyo ndivyo ilivyotokea, tunadhani ni bora tuelezee hilo kwenu.”

SOMA NA HII  KUELEKEA SIKUKUU HIZI....MTAANI CHIMBO LA PESA NI MOJA TU...NI AVIATOR YA MERIDIANBET...