Home Habari za michezo ZA NDANIII KABISAA….KWENYE ORORDHA YA MASTAA WAPYA SIMBA..MPOLE NAYE YUMO…WENGINE HAWA HAPA…

ZA NDANIII KABISAA….KWENYE ORORDHA YA MASTAA WAPYA SIMBA..MPOLE NAYE YUMO…WENGINE HAWA HAPA…


SIMBA usiku wa juzi ilikuwa uwanjani kumalizana na Ruvu Shooting, huku mabosi wake wakianza hesabu mpya kwa ajili ya msimu ujao, ikiwaweka kwenye rada zao nyota wawili wakali wa kutupia.

Uongozi wa klabu hiyo baada ya kubaini msimu huu wanaweza kutoka kapa katika Ligi Kuu, huku ikiwa imeshang’olewa kwenye michuano ya CAF, imeamua kumpa kocha Pablo Franco siku saba ili awasilishe ripoti yake wakiwa wamevutiwa na nyota wawili wapya.

Nyota hao ambao hata hivyo itategemea na uamuzi wa mwisho wa Pablo kutua Msimbazi ni George Mpole wa Geita Gold na Mkongoman mwenye uraia pia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cesar LobiManzoki anayecheza Mabingwa wa Ligi Kuu Uganda, Vipers.

Mpole ana mabao 12 akiwa kinara sambamba na Fiston Mayele wa Yanga, wakati

Mbali na hao tayari kiungo wa Dodoma Jiji, Cleophace Mkandala amebakiza hatua chache kabla ya kujiunga na timu hiyo kwa msimu ujao, ikiwa ni pendekezo la kocha huyo kutoka Hispania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kuwa, wametaka kocha Pablo kuwapa ripoti na tathmini yake kwa ajili ya msimu huu na mipango ya msimu ujao ikiwamo usajili ili waanze mambo mapema.

Try Again alisema baada ya kufahamu nafasi anazotaka kuongezewa nguvu, wachezaji wapya aliyovutiwa nao na timu wanazotoka ili kuona namna gani tunaanza mchakato wa haraka kuwatafuta na kuwapata.

Alisema kila eneo ambalo atakuwa anataka mchezaji mpya kutakuwa na machaguo si chini ya mawili ili tukimkosa wa kwanza kuona namna gani tunafanikiwa kumchukua mwingine kulingana na mahitaji yake yalivyo.

“Ripoti yake itatueleza kama kuna wachezaji anataka wapunguzwe pamoja na masuala mengine ya kiufundi ili timu yetu iweze kufanya vizuri zaidi msimu ujao yote hayo yapo chini yake,” alisema Try Again na kuongeza;

“Wakati huu hatuwezi kueleza tutasajili wachezaji wangapi hadi hapo Pablo atakapo tupatia ripoti yake ikiwemo kutueleza na suala lake la kuhusishwa na Orlando Pirates ila niwahakikishie tutaleta wachezaji wapya wa maana.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUMZUIA WAWA ASINGIE UWANJANI...PABLO AVUNJA UKIMYA...ATOA LAWAMA...

“Tusubiri Pablo atupatie uongozi kile anachohitaji kwenye ripoti yake tutajadili na tutamtimizia kwa kiasi kikubwa atakavyokuwa anahitaji ili kuona timu inaongezeka makali na kufikia malengo yetu makubwa.”