Home Habari za michezo ETO’O AMKAZIA MATIP KUJIUNGA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON….’KAMPA ZA USO’ KISA...

ETO’O AMKAZIA MATIP KUJIUNGA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON….’KAMPA ZA USO’ KISA ALIIKIMBIA TIMU WAKATI WA SHIDA…


GWIJI wa soka Duniani, Bara la Afrika na Rais wa Chama cha Soka cha Cameroon Samuel Eto’o amekatalia katakata beki wa Liverpool na raia wa Cameroon Joel Matip kuhusu maombi yake ya kujiunga na Timu ya Taifa ya Cameroon ili aweze kushiriki Fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Qatar.

Mnamo mwaka 2016 Matip alitangaza rasmi kustaafu kuchezea timu ya Taifa ya Cameroon huku akitoa sababu kuwa uongozi mbaya na changamoto anazokutana nazo akiwa timu ya Taifa ndizo zilizomfanya achukue uamuzi huo.

“Nadhani kwa sasa inatosha na naangalia mbele,nilichokitaka ni kubaki hapa(Liverpool) na kucheza.” Alisema Matip mnamo mwaka 2017.

Lakini baada ya hivi karibuni Timu ya Taifa ya Cameroon kujikatia tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar chini ya utawala wa Samuel Eto’o kama Rais wa Chama cha Soka cha nchi hiyo, taarifa zikaibuka kuwa Matip alituma maombi ya kujumuisha kwenye kikosi hicho ili apate fursa ya kushiriki Kombe la Dunia na haya ndiyo yalikuwa majibu ya Eto’o:

“Hii ni timu ya Taifa hatuvumilii watu ambao wanajiona wao ni muhimu sana, wanaotaka kujumuika nasi pale wanapoona asali na matunda, tulipambana wenyewe na tunayo heshima kubwa kwa wachezaji ambao walilipambania Taifa hili katika nyakati mbaya na nyakati nzuri. Hata mimi mwenyewe nimewahi kuwa kwenye timu bora duniani lakini sijawahi idharau Simba Wateranga, nadhani muda wa Matip umeshapita inatakiwa aichezee Liverpool daima, wale walioianza kazi hii lazima wakaimalizie Qatar. Haijalishi ni kina nani lakini lazima waende Qatar wakafurahie matunda yao ya kufuzu. Hakuna mtu atakayekula matunda yao bali ni wao wenyewe.” Alisema Eto’o.

Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kufanyika nchini Qatar mwishoni mwa mwaka huu.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWATUNGUA WAARABU JANA...RAIS SAMIA AWAPA KONGOLE YANGA....