Home Habari za michezo IMEFICHUKA…KUMBE PABLO HAKUTAKA CHAMA ASAJILIWE SIMBA….’KIBOSILE ALIMSAJILI KINGUVU KWA MAHABA YAKE.’..

IMEFICHUKA…KUMBE PABLO HAKUTAKA CHAMA ASAJILIWE SIMBA….’KIBOSILE ALIMSAJILI KINGUVU KWA MAHABA YAKE.’..


MWAMBA wa Lusaka, Clatous Chama hakutakiwa kusajiliwa ndani ya kikosi cha Simba msimu huu wa 2021/22 na badala yake alitakiwa kusajiliwa mshambuliaji wa kazi ambaye angetatua tatizo la ubutu wa ushambuliaji.

Kiongozi mmoja wa Simba ambaye yupo ndani ya kamati inayofanya masuala ya usajili ameeleza kuwa ni mapendekezo yaliyofanywa na mtu mmoja pekee ambaye alitaka Chama asajiliwe.

“Chama ni mchezaji mzuri lakini hakuwa kwenye mpango wa kusajiliwa Simba hasa ukizingatia kwamba tayari RS Berkane alikokuwa akicheza amecheza mashindano ya kimataifa hivyo asingekuwa na nafasi ya kucheza kwa mara nyingine akiwa Simba.

“Kurejea kwake ni shinikizo la kiongozi mmoja ambaye alikuwa anahitaji kiungo huyo arudi na amerudi hakuna ambacho amekifanya zaidi ya kushughulikia matatizo ya kifamilia pamoja na kuwa anatibu majeraha.

“Ripoti ya Kocha Didier Gomes ambaye aliondoka pamoja na huyu Pablo Franco ambaye amefukuzwa ilikuwa inahitaji mshambuliaji wa kazi akaletwa kiungo hivyo ndio maisha yalivyokuwa na sasa hakuna kinachoendelea,” ilieleeza tarifa hiyo.

Kwa sasa Pablo amefutwa kazi ndani ya Simba kutokana na kushindwa kuipa taji la Ligi Kuu Bara kwa kuwa wameachwa na watani zao wa jadi Yanga kwa pointi 13 jambo ambalo linahitaji maajabu kwao kuwa mabingwa.

Kutolewa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho na Yanga kumewafanya pia wasiwe na matumaini ya kutwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa kuwa hawatacheza fainali Julai 2,2022 ila itakuwa ni Yanga v Coastal Union.

Kuhusu hilo hivi kariuni Rais wa Heshima ndani ya Simba, Mohamed Dewji alisema kuwa lazima wafanye maamuzi magumu kwa ajili ya timu hiyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAHENYESHA SIMBA...MINZIRO ADAI SIMBA NI WA DAKIKA 30 TU..BAADA YA HAPO NI MDEBWEDO..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here