Home Habari za michezo KAIZER CHIEF WAIZIDI UJANJA SIMBA KWA STARIKA LA MAGOLI KUTOKA CAMEROON…’WAINGILIA TREN...

KAIZER CHIEF WAIZIDI UJANJA SIMBA KWA STARIKA LA MAGOLI KUTOKA CAMEROON…’WAINGILIA TREN KWA MBELE’…


JUNI 3 mwenzi huu gazeti la Mwanaspoti liliripoti kuhusiana na Klabu ya Simba Sc kumuweka kwenye rada za usajili straika Mcameroon, Frank Mbella Etouga anayekipiga Asante Kotoko ya Ghana alijiunga mwaka jana ambaye rekodi zake zinaonyesha katika mechi 28 amefunga mabao 21.

Sasa chanzo cha habari nchini Afrika kusini kimeripoti kuwa klabu ya Kaizer Chief tayari imeshaanza kufanya mazungumzo na Straika huyo huku wakiongeza kuwa wababe hao wanaweza kukamilisha usajili huo hivi karibuni ikiwa watafikia kiasi wanachokihitaji Asante Kototo.

Simba wanaweza kumpoteza Straika huyo aliyezaliwa nchini Cameroon mwaka 2001 ambapo hadi sasa ameshapita kwenye klabu mbalimbali ikiwemo Fortuna du Mfou ya Cameroon kabla ya kujiunga na timu yake ya sasa octoba 18 mwaka jana.

Frank Mbella Etouga anatajwa kwenda kuziba pengo la Leonardo Castro ambaye anamaliza mkataba wake ndani ya Kaizer Juni 30 mwezi huu ikiwa ni moja ya usajili kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Kaizer Chief ya Afrika Kusini tayari imewaacha wachezaji wake 10 na sasa Viongozi na Maboss wa timu hiyo wameingia sokoni koboresha kikosi chao ambapo kwasasa kinaongozwa na kocha Arthur Jabulani Zwane.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KANOUTE....SIMBA SC WAVUNJA UKIMYA KUHUSU YANAYOENDELEA JUU YAKE...