Home Habari za michezo KIUNGO WA SIMBA AKATALIWA SINGIDA BIG STARS…WADAI HAYUPO KWENYE MAFAILI…

KIUNGO WA SIMBA AKATALIWA SINGIDA BIG STARS…WADAI HAYUPO KWENYE MAFAILI…


Klabu ya Singida Big Stars, imekanusha tetesi za kuwa kwenye mpango wa kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Kenya Harrison Mwendwa, ambaye aliwasili jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita.

Klabu hiyo ambayo itashiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao (2022/23), imehusishwa na mpango wa kumsajili Mwendwa, baada ya kudaiwa dili lake la kusaini Simba SC limevunjika.

Afisa Mtendaji mkuu wa Singida Big Stars Muhibu Kanu amesema hawana mpango wa kumsajili Mshambuliaji huyo, na wanashangazwa kuona klabu yao imeingizwa kwenye tetesi hizo.

“Hatuna mpango wa kumsajili Mwendwa, kwenye mafaili yangu hakuna kitu kama hicho, unajua wakati huu wa tetesi kila mtu anazungumza lake, lakini niamini mimi kama mtendaji mkuu hakuna mpango wowote wa kumsajili huyu mchezaji.” Amesema Muhibu Kanu.

Kwa sasa inadaiwa kuwa Mwendwa amesharejea nchini kwao Kenya, na anasubiri dili lingine kutoka kwenye klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushindwana na Viongozi wa Simba SC ambao wamedhamiria kufanya maboresho kwenye kikosi chao katika kipindi hiki cha usajili.

SOMA NA HII  KIPIGO CHA JANA CHAZIDI KUWAZUZUA WAARABU...WAMSHITAKI MWAMUZI CAF..WADAI ALIHONGWA NA SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here