Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…MO DEWJI AJA NA STAILI YA FAGIO…AFUNGUKA KIMAFUMBO WANAOHUSIKA…TRY AGAINI...

KUELEKEA MSIMU UJAO…MO DEWJI AJA NA STAILI YA FAGIO…AFUNGUKA KIMAFUMBO WANAOHUSIKA…TRY AGAINI AKAZIA…


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu na Kombe la Azam Sports, Simba SC wanamaliza msimu vibaya kwa kushindwa kutetea mataji yake waliyobeba msimu uliopita.

Simba inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama 51 baada ya kushuka dimbani michezo 25, alama 13 nyuma ya vinara Yanga wenye alama 64.

Kombe la Azam Sports Simba walitolewa hatua ya Nusu Fainali na Yanga Mei 28 kwa goli la Kiungo Feisal Salum.

Kwa upande wa Michuano ya Kimataifa Simba walitolewa hatua ya Robo Fainali na Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini.

Sasa kwa Anguko hilo la Wekundu hao wa Msimbazi kwanza walianza kumtimua Kocha Pablo Franco baada ya kushindwa kutimizamatakwa ya Mkataba wake ikiwa ni kutetea mataji hayo mawili na kufika hatua ya nusu Fainali Michuano ya CAF.

Kutimuliwa kwa Kocha Pablo wengi walilalamika ni makosa kwa kuwa alipaswa kupewa muda na badala yake baadhi ya wachezaji ambao hawaendani na kiwango cha klabu hiyo kwa sasa walipaswa kuachwa.

Sasa Kumbe kubwa zaidi ni kuwa Simba wamejipanga kusafisha kila eneo ambalo uongozi unadhani kuna tatzo ili kujiandaa vyema na msimu unaokuja.

Hii inakuja baada ya Rais wa Hishima na Mwekezaji ndani ya Klabu hiyo, Mohammmed Dewji kupost Picha katika mtandao wake wa Twitter na kuudindikiza na Maneno;

“Tunasafisha kila sehemu ambayo inahitaji kuwekwa sawa ili turudi kwenye ubora wetu”

Mbali na hilo mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Klabu ya Simba Salim Abdallah “Try Again” amedokeza kuwa Mo Dewji amerudi kwa ajili ya kutoa sapoti kuelekea dirisha lijalo la usajili.

Tazama tweet ya “Mo” hapa chini;


SOMA NA HII  BANGALA NA DJUMA WAPIGWA PINI YANGA...ISHU YAO YA KWENDA SIMBA YAFIA MEZANI...