Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KUSEPA TENA SIMBA….CHAMA AVUNJA UKIMYA…”UONGOZI UFANYE MAAMUZI…NITAANZA MAISHA MENGINE”…

KUHUSU ISHU YA KUSEPA TENA SIMBA….CHAMA AVUNJA UKIMYA…”UONGOZI UFANYE MAAMUZI…NITAANZA MAISHA MENGINE”…


HUKO Msimbazi baadhi ya mashabiki wa Simba waliingia ubaridi baada ya kusikia tetesi, Clatous Chama ndo basi tena hasa baada ya kuondolewa kikosini na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pablo Franco kabla ya mechi ya nusu fainali ya Kombe la ASFC.

Hata hivyo, kiungo huyo amevunja ukimya na kutoa msimamo wake, akisema kwa msisitizo, ‘bado yupo sana Simba’, kisha kuwatuliza mashabiki hao kwa kuwaambia mchana wa leo atatua jijini Dar kutoka Zambia ili kuwapa furaha kwenye mechi zilizosalia za Ligi Kuu Bara.

Chama aliondoka siku chache katika kambi ya Simba iliyokuwa jijini Mwanza kabla ya mechi dhidi ya Yanga ambayo Simba ilicharazwa bao 1-0 kwa maelezo anasumbuliwa na majeraha, pia ikielezwa aliomba ruksa ya mapumziko kwa sababu ya matatizo ya kifamilia ikiwamo kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha mkewe, Mercy Chama aliyefariki dunia Mei 29, 2021.

Hata hivyo, huku nyuma katika mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa nyingi ikiwamo jamaa ndo basi tena Msimbazi, lakini jana akizungumza  kutoka Lusaka Zambia, Chama alisema leo mchana anatua Dar na wanaotamani asepe klabu hapo watasubiri sana.

Kiungo huyo alisema kumekuwa na mambo mengi yanayozungumzwa huku nyuma dhidi yake lakini kati ya hayo hakuna hata moja lililokuwa la kweli kwa upande wake na hafahamu kitu.

Alisema baada ya kufika Tanzania moja kwa moja ataungana na timu kulingana na ratiba ilivyo na bado yupo sana Msimbazi, labda kama mabosi wa klabu hiyo wataamua kumtoa wao.

“Uongozi wa Simba labda wao ndio ufanye maamuzi hayo, ila kutoka kwangu hakuna kitu kama hicho, narudi kwa ajili ya kuipigania timu yangu na kuhakikiha tunamaliza vizuri kwa kupata ushindi mechi zote tano zilizokuwa mbele yetu,” alisema Chama na kuongeza;

“Nipo kwenye mkataba wa muda mrefu na Simba, mchezaji halali wa timu hii hilo ndio nalifahamu hakuna lingine lolote zaidi ya hapo labda kama nitaambiwa baada ya kufika Tanzania.

SOMA NA HII  RASMI....MBAPPE AFUNGUKA SAKATA LAKE NA NEYMAR...AKIRI KUNA MGOGORO KISA MESSI NA PSG....

“Unajua kila mchezaji lazima uwe na malengo katika maisha ya soka akili yangu ipo hapa Simba kuifanyia makubwa zaidi kama ambavyo wamewekeza kwangu kama kutakuwa na mabadiliko mengine au jambo lolote nitaanza maisha mengine.”

Juu ya maendeleo yake ya jeraha la mguu Chama alisema; “Binafsi maendeleo ya afya ni mazuri nitafanya vipimo vya mwisho na madaktari wangu wa Simba kwa jinsi nilivyo naimani watanipa ruhusa ya kuendelea na mazoezi pamoja na kucheza mechi.”

Uongozi wa Simba ilimpa Chama mapumziko ya kwenda kwao Zambia kukamilisha masuala yake ya kifamilia pamoja na kuendelea na matibabu ya majeraha yake ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua kabla ya kuondoka nchini.

Akiwa na kikosi cha Simba, Chama baada ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili amefunga mabao manne na kutoa pasi ya mwisho moja kwenye kombe la Shirikisho (ASFC).

Chama katika Ligi Kuu Bara licha ya kucheza mechi chache kutokana na majeraha, kujiunga na timu nusu msimu amefunga mabao matatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here