Home Habari za michezo MORRISON ATHIBITISHA KURUDI TENA BONGO….YANGA WATAJWA KUWA NYUMA YA MCHEZO MZIMA….

MORRISON ATHIBITISHA KURUDI TENA BONGO….YANGA WATAJWA KUWA NYUMA YA MCHEZO MZIMA….


Aliekuwa mchezaji wa Simba SC, Bernard Morisson amethibitisha kurejea Tanzania hivi karibuni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram (Insta Story) Bernard Morrison amethibitisha kuwa yupo njiani kurejea Tanzania

Ikumbukwe kuwa nyota huyo alipewa mapumziko na Simba Sc pamoja na kuagwa/kutakiwa kila la heri katika maisha yake mapya ya soka.

Taarifa zinasema Morisson yuko mbioni kurejea Klabu yake ya zamani Yanga, na tayari ameshamalizana na matajiri wa Klabu hiyo.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Morrison kuichezea Yanga endapo dili hilo litafanikiwa ,ambapo anatazamiwa kuziba pengo lililoachwa wazi na Saido Ntibazonkiza ambaye naye ameshaagwa ndani ya Mabingwa hao watarajiwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.

SOMA NA HII  GAMONDI AWAWEKEA MKAKATI WA HATARI KMC LEO