Home Habari za michezo RASMI….MANARA AMATAMBULISHA MORRISON YANGA…ATUMIA NJIA YA ‘KININJA’ KWA KUMTAJA KUWA MCHEZAJI BORA….

RASMI….MANARA AMATAMBULISHA MORRISON YANGA…ATUMIA NJIA YA ‘KININJA’ KWA KUMTAJA KUWA MCHEZAJI BORA….


MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema kuwa kulingana na mafanikio waliyokuwa nayo klabu ya Yanga msimu huu kikosi bora cha msimu kwa mtazamo wake kinatakiwa kiwe na wachezaji zaidi ya 7 hadi 9.

Msemaji huyo ameongezea kwa kusema kuwa mchezaji wa Simba Bernard Morrison naye anastahili kuwemo kwenye kikosi hicho licha ya kucheza michezo michache ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Alipoulizwa kwanini Bernard Morrison, wakati amecheza michezo michache? Manara alijibu kuwa Bernard Morrison ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee na ubora mkubwa unaomfanya aingie kwenye kikosi hicho.

Hata hivyo, habari za uhakika ni kuwa tayari Yanga wameshamalizana na Morrison, ambapo kilichobaki ni kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania.

Morrison anatarajiwa kutangazwa Yanga Mwishoni mwa msimu huu, ili kuiepusha klabu hiyo na malipo ya kuvunja mkataba baina yake na Simba.

Kwa mantiki hiyo, Manara anawaandaa kisaikolojia mashabiki wa Yanga kuwa wajiandae kwani nyota huyo kuanzia msimu ujao ni mali yao.

SOMA NA HII  KILA KURASA MOJA YA 'POWER MERLIN MEGAWAYS' INAKUHAKIKISHIA USHINDI 'DAILEEE'....