Home Habari za michezo SAFARI YA KAMBI MAREKANI YAZIDI KUNUKIA YANGA….GSM AGOMA KURUDIA YA MOROCCO MWAKA...

SAFARI YA KAMBI MAREKANI YAZIDI KUNUKIA YANGA….GSM AGOMA KURUDIA YA MOROCCO MWAKA JANA…


ILE kambi ya Yanga kule Boston, Marekani sasa imeiva! Mabosi wa timu hilo wapo kwenye mchato wa mwisho wa kushughulikia viza. Yanga inayohitaji pointi tatu tu kabla ya kutangaza mapema ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, huku ikiwa imetinga fainali za ASFC itayoumana na Coastal Union, Julai 2 jijini Arusha itaondoka kwenda Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano.

Yanga inakwenda kuweka kambi hiyo baada ya ahadi kutoka kwa GSM ambaye aliwaahidi tangu mwaka jana kutokana na maandalizi mabaya ya kambi ya Morocco msimu uliopita. 

Hawataki kurudia makosa msimu huu wameamua kujipanga mapema ili muda ukifika mambo yote yawe sawa juzi Jumatatu mastaa wote waliambiwa wawasilishe nyaraka zao za kusafiria kwa maandalizi ya kuomba viza katika ubalozi wa Marekani kwa maelezo mchakato wake unachukua muda mrefu.

“Tumeambiwa tuwasilishe hati zetu zote ili kuanza maandalizi ya kutafutiwa viza,” alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga aliyeomba kuhifadhiwa jina.

Mbali na Marekani ambalo ni chaguo la kwanza la bilionea huyo wa Yanga, pia yapo machaguo mengine mawili ikiwamo Uturuki na Afrika, huku Sauzi ikiwa pia kwenye orodha kama mambo yatakwama.

Wakati huohuo Yanga juzi Jumanne walimenyana na Friends Rangers kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Avic Town Kigamboni na kuibuka na ushindi wa mabao 8-0.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yalifungwa na Yusuf Athumani matatu, Heritier Makambo mawili, Denis Nkane mawili na Fiston Mayele moja.

Mchezo huo ulikuwa maalum kwaajili ya kujiweka fiti tayari kwaajili ya michezo iliyobaki ambao wachezaji waliocheza mchezo huo ni wale ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa.

Mbali na mchezo huo Yanga watacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja huohuo siku ya Jumamosi jioni.

SOMA NA HII  KOCHA STARS AMRUDISHA FEISAL SALUM "FEI TOTO" YANGA...ANOLEWA KUKIWASHA KIMATAIFA