Home Habari za michezo SIMBA WAENDELEA KUIKIMBIZA YANGA MICHANGO YA NANI ZAIDI…BUMBULI ASHTUKIA ‘JANJA JANJA’ YA...

SIMBA WAENDELEA KUIKIMBIZA YANGA MICHANGO YA NANI ZAIDI…BUMBULI ASHTUKIA ‘JANJA JANJA’ YA UPANDE WA PILI….


Klabu ya Simba imesema hakuna wa kuwazuia kuendelea kutekeleza programu uzao za maendeleo.

Kauli hiyo ya Simba imekuja baada ya mwitikio mzuri wa mashabiki wakionesha kuchangia kwa wingi fedha katika shindano la nani zaidi.

Shindano hilo lilizinduliwa na klabu hizo mbili hivi karibuni kwa lengo la kuhamasisha mashabiki wao kuwachangia fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Wakati Simba ikijivunia namna mashabiki wanavyojitoa kuchangia, Yanga imesema imeanza harakati za kuhamasisha mashabiki na wanachama ndani ya makundi ya mitandao ya kijamii ya ‘WhatsApp’ kuchangia baada ya mwitikio kuwa mdogo.

Takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na wadhamini wa klabu hizo Azam Media zinaonesha Simba ikipiga hatua kubwa ikielekea kwenye Sh milioni 100 huku Yanga ikiwa imeachwa pa kubwa kwenye Sh milioni 40 kuelekea 50.

Akizungumzia mipango yao Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu alisema mwitikio wa mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba unawapa matumaini ya kuendelea na mipango yao ya maendeleo kama walivyopanga na kuwapongeza wote wanaoshiriki kuchangia.

“Naamini kabisa wiki inayofuata tutatoa programu nyingine kubwa ya maendeleo, tunawashukuru wanachama na mashabiki wa Simba kwa kuendelea kuunga mkono timu yetu na mpaka sasa fedha ni nyingi,”alisema.

Alisema Simba imekuwa na chachu ya kufanya shughuli za maendeleo kwani wamenunua uwanja wenyewe na wameuendeleza na kwamba programu yao ni kufanya ujenzi wa majukwaa.

Mangungu alisema watu wamekuwa wakizungumzia suala la uwanja katika hali ndogo na kusahau kuwa mwekezaji alishaweka Sh bilioni mbili, na kwamba wao wanaamini wako katika nafasi nzuri na watakusanya fedha za kutosha na wala hakuna mtu atakayewasitisha katika mipango hiyo.

Kwa upande wa Yanga Msemaji wake Hassan Bumbuli alisema wenzao Simba wameongoza kwasababu waliweka nguvu kubwa wakati wao walikuwa wamebanwa na majukumu mengine ya kutangaza uchaguzi lakini wamerudi upya wakihamasisha mashabiki wao kuchangia.

Alisema wanatarajia kuchanga kwa nguvu zote kupitia vikundi zaidi ya 200 vya Yanga kuhakikisha wanachanga kwa wingi ili kuwapita wapinzani wao .

SOMA NA HII  DAH...CHAMA NDIO BASI TENA ....AFUNGUKA SHIDA ANAYOIPITIA SIMBA...HATACHEZA KWA MWEZI MZIMA...

“Mbinu yetu ni kuwashirikisha wanachama kupitia vikundi vya WhatsApp, ili tukienda kuutafuta ubingwa tuwe na furaha ya kuchukua taji la Ligi Kuu na ya kuongoza kwa mapato,”alisema.